Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, November 6, 2014

NAIBU KATIBU MKUU CHADEMA ZANZIBAR,SALUM MWALUM, ATEMA CHECHE IYELA JIJINI MBEYA

Meza kuu katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu akifurahia jambo pamoja na viongozi wenzie.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema waliofurika kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Iyela jijini Mbeya.


 Sehemu ya Umati wa Wananchi wa Iyela.

Kwaya ya Chadema ikitoa burudani.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya mjini, John Mwambigija akihutubia wananchi.

Baadhi ya Walinzi wa Chadema wakiimarisha usalama eneo la mkutano.


 Mamia ya Wananchi wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu.





NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, amewasihi wakazi wa Jiji la Mbeya kuendelea kukiunga mkono Chama hicho katika chaguzi zijazo ili waweze kushika dola.

Mwalimu alitoa wito huo jana alipokuwa akihutubia mamia ya Wafuasi wa Chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Iyela Airport ya zamani jijini Mbeya.

Alisema ni vema wananchi wakalinganisha maendeleo waliyoyapata baada ya eneo lao  kuongozwa na Chadema na kabla ya hapo kisha wakatoa uamuzi sahihi katika chaguzi zijazo kwa kuendelea kukipa majimbo Chama hicho.

Mwalimu alisema Majimbo mengi ambayo Chadema inawabunge wake hali ya maendeleo inaenda kwa kasi kubwa sana tofauti na awali ambapo majimbo hayo yalishikiliwa na CCM na kuongeza maeneo mengi ukusanyaji wa mapato umeongezeka kwa Wabunge hao kudhibiti mianya ya Halmashauri kuchakachua mapato.

Alitolea mfano Majimbo ya Mbeya mjini, Momba,Iringa Mjini, Mwanza na Arusha ambako alisema hakuna vitega uchumi vilivyoongezeka kabla ya uchaguzi na baada ua uchaguzi lakini ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri yanaongezeka kwa kasi kubwa.

Naye Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija alisema Chama chake kimejipanga kuhakikisha kinachukua mitaa yote 181 ya Jiji la Mbeya katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Disemba mwaka huu.

Mwambingija alisema wamejipanga kuchukua mitaa yote kwa kuwahamasisha wanachama wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kupigia kura ili siku ya uchaguzi wanachama wengi wawe na sifa ya kupiga kura.

Alisema vijana ndio wanapaswa kujitokeza kujiandikisha siku za mwanzo ili kuwazidi kete wapinzani wao ambao ni Chama cha Mapinduzi na kusisitiza kuwa siku ya kujiandikisha hata vijana wadogo chini ya miaka 18 ni vema wakatumia mwanya wa kudanganya umri ili waweze kupata idadi kubwa ya wanachama.

Aliongeza kuwa mikakati mingine tayari Chama kimewaandaa walinzi wake Red Brigedi kuhakikisha siku ya uchaguzi wanalinda maboksi ya kupigia kura ili kuepuka udanganyifu wowote unaoweza kujitokeza kwa wasimamizi wa uchaguzi.

Mwambigija alisema Redbrigedi wamepewa mafunzo maalumu ya kupambana na udanganyifu wowote kwa kuweza kuwadhibiti watendaji wa Mitaa watakaosimamia uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwaadhibu kwa vipigo kama itabainika.

Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments: