Msanii wa Muziki wa kizazi Kipya Bongo Fleva Shukrani Jaito(SJ) wa kwanza kushoto akiendelea na Mahojiano na Mwandishi wa Habari Venance Matinya
Mwandishi wa Habari Venance Matinya wa kwanza Kulia akichukua maelezo kutoka kwa Msanii wa Bongo Fleva Shukrani Jaito(SJ)
WADAU wa mziki wa kizazi kipya
maarufu kwa Bongofleva wametakiwa kuwapa nguvu wasanii wanaochipukia ili
kuwawezesha kufikia malengo na mafanikio
katika Tasnia ya kutoa elimu na burudani kupitia sanaa hiyo.
Wito huo umetolewa na msaanii
anayeibukia wa Jijini Mbeya, Shukrani Jaito(SJ) alipokuwa akizungumzia
changamoto anazokumbana nazo katika kusakla riziki kwenye tasnia ya Muziki wa
kizazi kipya katika Mahojiano maalumu na Mtandao Mbeya yetu Blog
Shukrani alisema changamoto
kubwa anayokabiliana nayo na ambayo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ni
kumuwezesha kufika katika studio kubwa ili aweze kurekodi nyimbo zake na
hatimaye kupigwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini.
Alisema pia anahitaji msaada wa
kupata mdhamni ambaye atakuwa msimamizi wa kazi zake, kumuandalia matamasha
pamoja na kumpa ushauri juu ya namna mbali mbali za kufanya ili aweze kuinua
kipaji chake hicho cha mzuki wa kizazi kipya.
Aidha ametoa shukrani kwa Jacob
Mwaisango aliyemsaidia kwa kiasi Fulani hadi ameweza kurekodi nyimbo tatu
pamoja na kumpa fedha kwa ajili ya matumizi madogo madogo ingawa peke yake
hatoweza hivyo anatoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo.
Akizungumzia historia yake
anaseme alianza kuwa na kipaji cha kuimba tangu akiwa shule ya msingi darasa la
Tano hali iliyowapelekea baadhi ya walimu kumbatiza jina la msanii lakini
hakuweza kurekodi nyimbo yoyote.
Alisema hivi sasa ana nyimbo
tatu ambazo alianza kurekodi wimbo wa kwanza mwaka 2012 unaoitwa Pesa chini ya
studio ya Moja moja recird iliyoko Ilemi, Wimbo wa Pili uliorekodiwa mwaka huu
unaoitwa Bila wewe pamoja na Mama alizorekodi H studio iliyopo Isanga jijini
Mbeya.
Alisema hivi sasa anajipanga
kurekodi wimbo mmoja na msanii mkubwa ambaye ndiye ndoto yake na anayefuata
nyayo zake, Ali Kiba hivyo anaomba wadau kumsaidia kwa hali na mali ili aweze
kukutanishwa na msanii huyo pamoja na fedha za kuingilia studio.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment