Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, July 24, 2014

UCHANGIAJI WA FEDHA ZA MAANDALIZI NANENANE MBEYA WASUASUA.

 Meza kuu ya kikao cha maandalizi ya nanenane Kandaya nyanda za juu kusini ikisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa na wajumbe.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Deodatus Kinawiro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya na Mwenyekiti wa kikao cha maandalizi ya Nanenane akisisitiza jambo kwa wajumbe waliohudhuria kikao hicho.
 Mmoja wa Wajumbe wa Sekretarieti ya Nanenane Kanda, Hamza Mvano, akiwasilisha mada katika kikao cha maandalizi ya nanenane.

 Wajumbe wa kikao cha maandalizi ya nanenane 2014 wakifuatilia kwa makini yaliyoandikwa kwenye makabrasha wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa JKT Nanenane.
***********
MAANDALIZI ya Sherehe za sikukuu za wakulima nanenane Kanda ya Nyanda za juu Kusini bado yanasuasua licha siku kubakia chache kutokana na kukosekana kwa fedha.
 
 
Hayo yalibainishwa jana na Mjumbe wa Sekretarieti ya Nanenane Kanda, Hamza Mvano, wakati wa kikao cha mwisho cha maandalizi ya sherehe hizo kilichofanyika katika ukumbi wa JKT uliopo ndani ya Viwanja vya John Mwakangale Uyole jijini Mbeya.
 
 
Mvano alisema hadi kufikia Julai 24, mwaka huu idadi ya wadau waliothibitisha kushiriki maonesho ya mwaka huu imefikia 363 kati ya 399 waliopewa mwaliko.
 
 
Alisema mbali na washiriki kutokamilika lakini bado michango kwa ajili ya kufanikisha maonesho na sherehe za Kanda kwa mwaka huu imefikia kiasi cha shilingi Milioni 16.5 wakati malengo ni kukusanya Shilingi Milioni 181.
 
Alisema makusanyo hayo ni sawa na asilimia 9 hivyo kutia shaka kufanyika kwa ufanisi katika maonesho hayo licha ya wadau ambao ni Halmashauri na Ofisi za Makatibu tawala wa Mikoa kupewa taarifa mapema za uchangiaji.
 
Alivitaja viwango ambavyo vinavyotakiwa kuchangwa na Halmashauri kuwa ni Shilingi Milioni mbili kila moja na Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa shilingi Laki tano.
 
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikao hicho, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Deodatus Kinawiro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, alisisitiza Halmashauri zote kuhakikisha zinamalizia michango yao mapema kama wanavyopaswa.
 
Alisema ni aibu kwa mikoa ya Kanda ya Nyanda za juu kusini kushindwa kufanya maonesho kutokana na ukosefu wa fedha wakati Mikoa hiyo husifika kitaifa kwa uzalishaji mkubwa na kuongoza katika kuchangia pato la Taifa.
 
 
Maonesha hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika viwanja vya John Mwakangale Uyole jijini Mbeya huandaliwa na Chama cha Wakulima Tanzania (TASO).
 
Akizungumzia maandalizi ya mwaka  huu, Katibu wa TASO kanda ya Nyanda za juu kusini, Ramadhani Kiboko, alikiri kusuasua kwa maandalizi ya sikukuu za wakulima nanenane mwaka huu tofauti na miaka iliyopita.
 
 
Kiboko alisema kawaida kila mwaka maandalizi na shamla shamla za washiriki kuanza kuandaa maeneo yao pamoja na vipando huanza Juni 30 lakini hadi sasa hakuna kinachofanyika pamoja na jitihada za kuanza kutumika kwa stendi mpya.
 
 
Alisema tangu mwezi Machi mwaka huu TASO ilitoa barua za mialiko ya kushiriki maonesho ya mwaka huu kwa washiriki 399 ambao ni pamoja na Halmashauri za Kanda, Taasisi za Serikali, bodi za mazao, Taasisi za majeshi,Wizara za Serikali na vituo vya utafiti.
 
 
Pia alitoa wito kwa wafanyabiashara mbali mbali kutumia Uwanja wa John Mwakangale katika biashara zao kwa kuendeshea magulio au minada ya bidhaa mbali mbali kipindi ambacho kunakuwa hakuna maonesho.
 
Na Mbeya Yetu
 

No comments: