Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, June 23, 2014

FAMILY DAY YA TBL MBEYA YAFANA, WAFANYAKAZI WAJUMUIKA NA FAMILIA ZAO.

Meneja wa Kampuni ya Tbl, Wilaya ya Mbeya(District Manager),Vivianus Rwezaura,alisema lengo la siku hiyo ni kuwakutanisha pamoja wafanyakazi wa kampuni na familia zao ili kufahamiana na kubadilishana mawazo.
Moja ya watoto wa wafanyakazi wa kmpuni ya bia TBL akionyesha umahili wake wa kupiga danadana katika isku hiyo ya family Day
Mazoezi na michezo mbali mbali ilifanyika katika viwanja hivyo vya ifisi Mbeya
WAFANYAKAZI wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Mbeya wamefanya sherehe za familia zenye lengo la kuwakutanisha watumishi pamoja na familia zao ili kufahamiana na kubadilishana mawazo.

Sherehe hizo maarufu kwa jina la Family day zilifanyika juzi katika viwanja vya Hotel ya Ifisi iliyopo Mbalizi nje kidogo ya Jiji la Mbeya ambapo Wafanyakazi na familia zao walijumuika kwa pamoja katika michezo mbali mbali.

Akizungumza katika sherehe hizo,Meneja wa Kampuni ya Tbl, Wilaya ya Mbeya(District Manager),Vivianus Rwezaura,alisema lengo la siku hiyo ni kuwakutanisha pamoja wafanyakazi wa kampuni na familia zao ili kufahamiana na kubadilishana mawazo.

Rwezaura alisema kampuni huandaa sherehe kama hizo kila mwaka lengo likiwa ni kuzikutanisha familia na wafanyakazi pamoja na michezo mbali mbali kwa ajili ya kuimarisha afya za wafanyakazi na familia zao.

Nao baadhi ya watumishi wa kampuni hiyo walisema kitendo cha uongozi kuweka sherehe kama hizo ni kizuri kwa kuwa huzifanya familia za wafanyakazi kufahamiana kwa ukaribu pamoja na kuondoa tofauti zinazokuwa zimejengeka miongoni mwao.

Walisema suala la ufanisi wa kazi wa mtumishi huanzia kwenye ngazi ya familia ambapo akielewana vizuri na familia yake humfanya kuwa huru awapo kazini tofauti na mtumishi ambaye amekosana na familia yake hupelekea kufanya maamuzi mabaya awapo kazini.

Mwisho.

Na Mbeya yetu 

No comments: