[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
WATU
WAWILI WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA DIPLPOMA YA BUSSINESS ADMINISTRATION CHUO
CHA MZUMBE KAMPASI YA MBEYA, WAKAZI WA FOREST YA ZAMANI HOSTELI ZA NJE
WALIOTAMBULIWA KWA MAJINA YA 1. MICHAEL TARIMO
(20) NA 2. ALBERT SHENKALWA (23) WALIKUFA MAJI BAADA YA MTUMBWI
WALIOKUWA WANAUTUMIA KUPIGWA MAJI, KUPINDUKA NA WAO KUSHINDWA KUOGELEA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.05.2014
MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO
KATIKA ZOO YA WANYAMA ILIYOPO KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI – KATA YA SONGWE,
TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJIJINI. WANAFUNZI HAO WAKIWA NA
WENZAO 12 WALIKWENDA ENEO HILO KWA AJILI YA PICKNIC NA KUANGALIA WANYAMA NA BAADAE KWENDA KWENYE BWAWA
LINALOTUNZA SAMAKI NA KUANZA
KUINGIA NDANI YA BWAWA HILO KWA KUTUMIA MTUMBWI HUO KWA
ZAMU. KATIKA BWAWA HILO WATU HAWARUHUSIWA KUOGELEA ISIPOKUWA KUINGIA KWA
MTUMBWI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUWA MAKINI NA MAZINGIRA WANAYOKWENDA KUTEMBMELEA ILI KUEPUSHA MADHARA
YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
|
No comments:
Post a Comment