Serikali
imeanza kujenga Uwanja wa Michezo Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya utakaogharimu
zaidi ya shilingi bilioni 8.2 utaomilikiwa na Halmashuri ya Wilaya.
Mkuu wa
Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro amesema uwanja huo utakuwa na viwanja vitano
vya michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwanja wa mpira wa miguu,riadha,mpira
wa pete,mpira wa wavu na mpira wa kikapu.
Kinawiro
amesema hivi sasa waeunda kamati ya uhamasishaji wa ujenzi inayoongozwa na
Aidan Msigwa na mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 56
na wameanza kufyatua tofari za saruji kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa maduka
kuzunguka uwanja huo.
Aidha kapuni
ya saruji ya Mbeya(LAFARGE) wametoa mifuko 500 ya saruji kuunga mkono juhudi za
serikali wakati kampuni ya ujenzi wa Barabara kati ya Lwanjilo/Chunya wao watagharamia
kuutengeneza uwanja wa mpira wa miguu kwa kupanda nyasi na uwekaji wa magoli.
Mkuu wa
wilaya amesema fursa iko wazi kwa watu watakaokuwa tayari kujenga viwanja
vilivyosalia na mchango wao watauthamini na kuuweka kwenye kumbukumbu na
makampuni hayo yatatumia uwanja huo kujitangaza kibiashara.
Amesema ni
wakati mzuri kwa makampuni hayo kuwekeza katika sekta ya michezo hivyo kuyataka
makampuni yaliyoko wilayani Chunya na kwingineko kuitumia vema fursa hiyo kama
vile makampuni ya madini,vinywaji na makampuni ya simu za mikononi.
Hata hivyo
Kinawiro amewataka wananchi kila mmoja ashiriki kutoa mchango kwani mbali ya
kuwa kitega uchumi cha Halmashauri pia utatoa ajira kwa wakazi wa wilaya ya
Chunya hivyo kuondoa tatizo la ajira kwa vijana na kuwafanya vijana kuimarisha
afya zao kwa kushiriki michezo mbalimbali kwa viwanja vitakavyojengwa.
Wilaya ya
Chunya imeanza kukua kwa kasi baada ya Serikali kuanza ujenzi wa barabara ya
Mbeya/Chunya hali inayowafanya wawekezaji kuanza kuelekeza nguvu zao huko na
kutoa fursa kwa wakazi hao kukuza pato kwa wananchi.
Na Mbeya yetu
|
2 comments:
Mfanye kweli yasiwe maneno tu
UNAPOSEMA YASIWE MANENO KWANI NI WEWE NDIO ULIEWAULIZA KUUSU UWANJA?MSILETE MANENO YAKUKATISHA TAMAA
Post a Comment