Nawa mikono
Maadhisho ya
siku ya kunawa mikono duniani kila mwaka yatafanyika Mei 5 mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Humphrey Kihwelu amesema Mkoani Mbeya sherehe
hizo zitafanyika katika Hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa
kuwa ni Adrian Majembe Mwenyekiti wa Mtaa wa Block T Kata ya Iyela.
Kihwelu
amesema kuwa nia ya kufanya sherehe hiyo ni kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa
kunawa mikono kila wakati mara baada ya kutoka Hospitali na kabla na baada ya
kula chakula ili kuepukana na magonjwa ya maambukizi.
Kaimu Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa jamii kuhudhuria sherehe hizo ili kupata elimu juu ya
umuhimu wa kunawa mikono elimu itakayotolewa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Aidha
amesema Adrian Majembe ni mmoja wa wadau ambao wamekuwa mstari wa mbele kutoa
Elimu katika shule mbalimbali Mkoani Mbeya mpango ulionesha mafanikio makubwa.
Hospitali ya
Rufaa imekuwa mstari wa mbele kushiriki maadhimisho hayo ambapo mwaka jana
yalifanyika katika Hospitali ya wazazi ya Meta na Rufaa sherhe iliyopata
mafanikio makubwa baada ya wananchi waliohudhuria kunufaika na elimu
iliyotolewa.
Kihwelu
amesema mwaka huu wameanza maadhimisho hayo kwa kutoa elimu kwa Hospitali
mbalimbali za Serikali na Binafsi na kuonesha mafanikio.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment