Add caption
Timu ya
Taifa ya Malawi imefurahishwa na mapokezi mazuri waliyoyapata Mkoani Mbeya na
kuahidi kuonesha kandanda safi kati yake na timu ya Taifa(Taifa stars).
Kauli hiyo
imetolewa na Kiongozi wa msafara huo Mrs Flora Mwandira na kuungwa mkono na
Mwalimu mkuu wa timu hiyo Young Chimodzi aliyewahi kuichezea timu ya Taifa ya
Malawi kwa miaka kadhaa.
Mwandira
amesema Timu ya Malawi imewasili na msafara wa wachezaji 20 na viongozi 12 ambao
waliwasili siku ya alhamisi jioni na kufanya mazoezi katika uwanja wa Sokoine.
Mchezo huo
umevuta hisia za watu wengi umevuta hisia za wakazi wa Jiji la Mbeya na Mikoa
ya Jirani na kufanya nyumba nyingi za wageni kujaa.
Mwalimu wa
timu hiyo ameweka hadharani wachezaji waliwasili kupambana na Taifa Stars kuwa
ni Makipa Charles Swin na Richard Chipuwa na Walinzi Pirilani Zonda,Francis
Mulimbika,John Lanjesi,Emmanuel Zoya,Bashiri Maunde na George Nyirenda.
Wachezaji wa
kiungo ni pamoja na John Banda,Mecium Mhone,Douglas Chirambo,World
Nkuliwa,Frank Banda,Junior Chimodzi,Phillip Masiye na Ndaziona Chatsalira.
Washambuliaji
ni Gaston Simukonda,Green Harawa,Diverson Mlozi na Rodrick Gonani.
Kwa upande
wa chama cha mpira nchini kimetangaza kuwa kiingilio katika mchezo huo kitakuwa
ni shilingi 5000 na hakuna magari yatakayo ruhusiwa kuingia uwanjani isipokuwa
magari ya wachezaji,Polisi na Gari la wagonjwa na tiketi zitaanza kuuzwa saa
mbili asubuhi siku ya Jumapili katika vituo mbali mbali Jijini Mbeya.
Katibu wa Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya(MREFA)Seleman Harubu amewataka washabiki
kufika kwa uwingi uwanjani na kuishangilia timu yao ya Taifa kwa amani na
utulivu ili kuenzi heshima iliyopewa Mkoa wa Mbeya kwa TFF kukubali mchezo huo
kufanyika Mkoani hapa.
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment