Picha ya pamoja
Sherehe za
Maadhimisho ya kunawa mikono Duniani yameadhimishwa Mei tano mwaka huu katika
maeneo mbalimbali na Mkoani Mbeya yameadhimishwa katika Hospitali ya Rufaa na Mgeni rasmi alikuwa Adrian
Majembe.
Awali Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Daktari Humprey Kihwelo alieleza umuhimu wa
kunawa mikono kwa usahihi ikiwa ni juhudi za kuzuia magonjwa ya maambukizi kama
vile kuhara na magonjwa ya ngozi.
Kihwelo
amewataka wananchi wanaoingia na
kutoka katika Hospitali kunawa,pia wanapofamya shughuli mbalimbali wanawe
mikono ili kuepuka magonjwa ya maambukizi yanayotokana na uchafu.
Hata hivyo
Kihwelo alishukuru klabu ya Rotary kwa kutoa msaada wa vioski vya maji katika
milango ya Hospitali ya Wazazi ya Meta na Hospitali ya Rufaa ambavyo vinasaidia
watu wanaoingia na kutoka kuvitumia kunawa ambapo Hospitali inahudumia Sabuni
za kunawia bila kukosa.
Kwa upande
wake Mgeni Rasmi Adrian Majembe amesema kuwa jukumu la kunawa mikono lisiishie
kwa wageni wanaoingia na kutoka Hospitali bali pia wauguzi nao wanalo jukumu la
kunawa kabla na baada pindi
wanapowahudumia wagonjwa Hospitalini.
Pia Majembe
ambaye ni mmoja wa wadau wakubwa wa Sekta ya Afya amesema kuwa hivi sasa
wametoa elimu kwa wanafunzi zaidi ya 1000 Jijini Mbeya na maeneo ya Masoko na
ujumbe huo kupokewa vizuri ambapo umetoa matokeo mazuri.
Hivyo
amewataka wakazi wa Mbeya kuendelea kusambaza ujumbe huu ili kuendelea
kupunguza idadi ya wagonjwa wanaotokana na kutonawa mikono.
Majembe
amewashukuru klabu ya Rotary kwa msaada wao wa hali na mali ambapo katika
sherehe hizo klabu hiyo iliwakilishwa na Rais Mstaafu wa Mkoa Ephraim Njuu na
Rais wa Mkoa wa sasa Melas Mdemu amabao waeahidi kusaidia Serikali nafasi
inapopatikana.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment