Asia Hamisi akiwa amezirai mahakamani baada ya kuhukumiwa miaka mitano jela
Watu wawili
wa familia moja Frank Charles na mkewe Asia Khamis wamehukumiwa kifungo cha
miaka mitano jela au kulipa faini ya shilingi milioni moja kila mmoja kwa kosa
la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi.
Hakimu wa
mahakama ya wilaya ya Mbeya Maria Batulaine amewatia hatiani wanandoa hao baada
ya kuridhishwa na ushahidi usio
shaka wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka.
Imedaiwa na
Mwendesha mashitaka wa Serikali Juliana William amesema kuwa washitakiwa hao
walikutwa na kete 100 za bangi Novemba 19 mwaka jana eneo la Makunguru Jijini
Mbeya baada ya upekuzi wa Polisi.
Baada ya
kusikiliza pande zote mbili aliwapa washitakiwa nafasi ya kujitetea ambapo
walisema kuwa wana watoto wawili mmoja akiwa darasa la nne na mwingine akiwa
kidato cha tatu hivyo kuiomba mahakama kuwaangalia kwa jicho la huruma kwa kuwa
hilo ni kosa lao la kwanza.
Wakati
Hakimu Batulaine akitafakari adhabu kwa washitakiwa hao mshitakia wa pili Asia
Khamis alianguka ghafla kizimbani na kuzirai na kumwacha Hakimu akiwa kimya kwa
muda kabla ya kutoa hukumu.
Mwendesha
mashitaka Juliana William aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa
ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia ya kuvuta na kuuza madawa ya
kulevya.
Hakimu Maria
Batulaine aliwahukumu kwenda jela miaka mitano jela au kulipa faini ya shilingi
milioni moja kila mmoja na mshitakiwa wa kwanza alikuwa akihaha kutafuta fedha
hizo na baadhi ya wasamaria walikuwa wakitoa huduma kwa mkewe baada ya
kudondoka kizimbani na kuzirai.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment