HOMA YA DENGUE NI NINI?
Homa ya Dengue ni ugonjwa unaoenezwa kwa kuumwa na
mbu aina ya Aedes mwenye virus vya ugonjwa huu. Mbu hupata virusi vya homa ya
Dengue anapomuuma mtu mwenye ugonjwa huu.
Ugonjwa huu unaenezwa kutoka mtu mmoja kwenda
mwingine kwa kuumwa na mbu huyu.
DALILI:
Homa kali ya ghafla
Kuumwa kichwa hususani sehemu za machoni
Maumivu makali ya viungo na misuli ya mwili
Kichefuchefu au kutapika
Kutokwa na damu kwenye fizi, na sehemu za uwazi za
mwili.
Uchovu
ukimsikia ndugu au jamaa yako anasema kuwa na
dalili hizi muwahishe hospitali mapema.
#SAMBAZA
KUWASAIDIA NA WENGINE.
|
1 comment:
ahsante kwa lecture yako
Post a Comment