Mwenyekiti wa Klabu wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, Uswege Luhanga, alisema waandishi wanapaswa kuwa na umoja na mshikamano ili kuweza kujiletea maendeleo yao na klabu kwa ujumla.
|
Mwandishi mkongwe Meshack Njavike akisalimia vijana wake katika sherehe hizo |
Ni vigeregere na vifijo tu ukumbini |
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa
kuwa na vyanzo vingine vya mapato badala ya kutegemea shughuli za uandishi
pekee ili kuwa na urithi kwa familia zao na vizazi vijavyo.
Wito huo ulitolewa na Raisi Mstaafu wa
Muungano wa Klabu za waandishi wa habari(UTPC), Ulimboka Mwakilili, alipokuwa
akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari
duniani zilizoadhimishwa kwa Mkoa wa Mbeya kwenye ukumbi wa Itemba Green Village
uliopo Ilomba jijini Mbeya.
Mwakilili ambaye ndiye alikuwa mgeni
rasmi katika sherehe hizo zilizofana kupita kawaida alisema waandishi wa habari
wanapaswa kuwa wabunifu wa kuwa na miradi mingine itakayowasaidia kuongeza
vipato vyao na siyo kukaa na kusubiri posho kutoka kwa wadau.
Alisema wadau pia wanapaswa kuheshimu
kazi za waandishi wa habari kwa kuwatumia inavyotakiwa kwa kuzingatia maadili
na sheria za Nchi na siyo kumtumia mwandishi kwa maslahi binafsi.
Kwa upande wake Mgeni mashuhuri wa sherehe
hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alipongeza chama cha
Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya(MBPC) kwa kumheshimu na kumshirikisha katika
sherehe hizo.
Alisema ataendelea kushirikiana na
vyombo vyombo vya habari Mkoa wa Mbeya ili kuhakikisha hali ya amani na utulivu
inaimarika ndani ya Mkoa na kuufanya kuwa kivutio cha wageni na wawekezaji.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi,
Mwenyekiti wa Klabu wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, Uswege Luhanga,
alisema waandishi wanapaswa kuwa na umoja na mshikamano ili kuweza kujiletea
maendeleo yao na klabu kwa ujumla.
Katika maadhimisho hayo, Klabu ya
waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya ilifanya sherehe zake kwa kutanguliwa na
bonanza kubwa la michezo lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu
(TIA) Mafiati Mwanjelwa jijini Mbeya na baadaye sherehe ya Jioni kwenye Ukumbi
wa Itemba.
Akizungumzia Bonanza hilo, Mratibu wa
Sherehe hizo, Venance Matinya, alisema michezo mbali mbali ilichezwa na
washindi kukabidhiwa zawadi kutoka kwa viongozi wa Mbeya Press.
Aliitaja michezo hiyo kuwa ni pamoja na
mpira wa miguu ambao Timu ya Chama cha Wasanii Mkoa wa mbeya waliibuka kidedea
na kujinyakulia fedha taslimu shilingi Elfu hamsini(50,000/=), Mpira wa Pete
walishinda timu ya Kabwe Queens waliojinyakulia 20,000/=.
Michezo mingine ni kuvuta kamba,
kukimbiza kuku, kukimbia kwenye magunia, kutembea na yai na kuokota Fedha.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment