Kapteni wa timu ya Wenda akizungumza kwa furaha baada ya timu yake kuishinda timu ya Sido goli mbili kwa moja katika fainali za kumtafuta bingwa wa ligi ya Mkoa wa Mbeya. |
Mkurugenzi wa Wenda Sekondari akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na mashabiki wa timu hiyo. |
Baadhi ya mashabiki wa timu ya Wenda wakishangilia baada ya mpira kumalizika |
Wachezaji na mashabiki wa Wenda wakiendelea kushangilia kuwa mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Mbeya |
Wachezaji wa akiba wa timu ya Sido ya jijini Mbeya wakifuatilia kwa makini mchezo ukiendelea |
Mtanange ukiendelea katika uwanja wa Jeshi Mbalizi |
Katibu wa Mrefa Suleiman Haroub pamoja na wasimamizi wa ligi wakifuatilia kwa makini mchezo huo |
Wazee wa kazi wakiwa vitani na lazima mshindi apatikane. |
TIMU ya Mpira wa miguu ya Wenda yenye
makao yake makuu Mbalizi Wilaya ya Mbeya mkoani hapa imefanikiwa kuibuka bingwa
wa ligi ya Mkoa wa Mbeya baada ya kuibwaga Timu ya Sido ya jijini Mbeya katika
fainali iliyopigwa mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Jeshi Mbalizi.
Timu ya Wenda iliibuka kidedea na kuwa
bingwa wa Mkoa wa Mbeya baada ya kuibuka na magoli mawili kwa moja dhidi ya
Timu ya Sido ambapo magoli ya timu ya Wenda yalifungwa na Ally Kheri dakika ya
11 ya mchezo kwa adhabu ndogo iliyojaa wavuni moja kwa moja.
Dakika ya 48 ya mchezo huo Bahati
Mwashiuya aliifungia timu yake goli la pili baada ya kuwazidi kasi walinzi wa
timu ya Sidon a kuwafanya washambuliaji wa Timu ya Sido kuongeza kasi wakitaka
kusawazisha magoli hayo na hatimaye kuibuka na ushindi.
Kasi ya washambuliaji wa Sido ilizaa
matunda katika dakika ya 85 ya Mchezo huo baada ya Mshambuliaji wake Daniel
Peter kuangushwa katika eneo la hatari wakati akielekea kumsabahi Mlinda
,mlango wa Wenda na hivyo Mwamuzi wa kati Ngole Mwangole kuamuru Mkwaju wa
penati upigwe.
Aidha mkwaju wa penati uliopigwa
kiufundi na Meja Mgome uliiandikia goli la kufutia machozi timu ya Sido
lililodumu hadi kipenga cha mwisho kutoka kwa mwamuzi Ngole Mwangole kutoka
jijini Mbeya Timu ya Wenda 2 na Sido 1.
Kwa upande wake mmiliki wa Timu ya Wenda
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Wenda na Mkuu wa Shule ya
Sekondari Mbalizi, Fidelis Mwampoma alisema matokeo hayo ni maandalizi mazuri
ya timu yake ambayo haijafungwa tangu kuingia katika mzunguko wa sita bora.
Alizitaja timu ilizoingia nazo katika
mzunguko huo na kushinda zote kuwa ni pamoja na Mchezo kati ya timu yake na
Biashara fc kutoka Chunya ambapo waliibuka kwa goli moja bila kitu, Dhidi ya
Tukuyu Star mabingwa wa ligi kuu wazamani Moja kwa sifuri, Mazombe fc
kutoka Kyela goli 2 kwa moja, Airport fc kutoka jijini Mbeya magoli matatu kwa
moja na Sido iliyotinga fainali iliyotokanayo Mbili kwa Moja.
Aliongeza kuwa ushindi huo unarudisha
furaha kwa mashabiki wa Wilaya ya Mbeya iliyopotea tangu miaka ya 1997 ambapo
Wilaya hiyo haikuwahi kutoa bingwa wa Mkoa wa Mbeya ambapo timu zilikuwa
zikitoka kwenye wilaya zingine.
Alisema mikakati yao ni kuhakikisha timu
ya Wenda inacheza ligi kuu na kufanya Mkoa wa Mbeya kuwa timu nyingine tishio
kama ilivyo Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment