Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, April 25, 2014

NEWS ALERT: HATIMAYE HALMASHAURI YA JIJI YATUA KUREKEBISHA BARABARA ENEO LA BLOCK T LEO

Baada ya waandishi wa Habari kutoka Mbeya yetu Blog na Bomba Fm Radio kutinga katika eneo la Block T ambapo kulikuwa na tatizo la Barabara kuwa Mbovu na kuanza kurekebisha jana, Hatimaye leo hii asubuhi Halmashauri ya Jiji kwa Kuona umuhimu Mkubwa wa Barabara hiyo na kwa kuzingatia kuwa Daladala sasa zinapita eneo hilo ikiwa ndio njia mpya, wamefika katika eneo hilo na kumwaga vifusi vya nguvu pamoja na nguvu kazi yao na kuanza kuitengeneza barabara hiyo kwa kasi ili kupisha Shuguli za daladala hizo kuendelea kutumia njia hiyo pamoja na wakazi wengine waishio na wanaopita maeneo hayo.

Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji wakiwa wanaendelea na kazi huku wakiweka mawe katika Mashimo na kuziba barabara hiyo ili iweze kutumika
Kazi ikiwa inaendelea kwa kasi
Kifusi kikiendelea kutumika kwa ajili ya kurekebisha eneo hilo ambalo lilikuwa limeharibika vibaya
Kazi ikiwa inaendelea kwa kasi
Bado wafanyakazi kutoka Jiji wanaendelea kurekebisha barabara hiyo
Hakuna kupumzika hapa ni kazi tuu
Kila mmoja akiwa bize kuhakikisha kazi inaisha mapema
Mmoja ya wafanyakazi wa Jiji akiwa ameshika Jiwe kubwa kwenda kuliweka katika Shimo kubwa ili paweze pitika vizuri bila usumbufu


Vijana kazini.. hapa marekebisho ya Barabara yakiendelea

Picha na Mbeya yetu

No comments: