Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, April 25, 2014

MAMA WANNE APELEKWA KATIKA KITUO MAALUMU NA WATOTO WAKE WAWILI WALIOBAKI KWA AJILI YA UANGALIZI.




Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Aisha Mtanda, alisema wameguswa na mazingira anayoishi mama huyo na kuamua kumpa uangalizi kwa miezi sita zaidi.

Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya wakimuaga mama wanne mara baada ya kupata matibabu ya watoto wake katika hospitali hiyo


Meneja wa Kituo cha Nuru, Amanda Fihavango alisema alikubali jukumu la kuwapokea watoto hao pamoja na mama yao kutokana na kuguswa na hali iliyowakuta ya kupotea kwa watoto wawili kati ya wanne.









UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kupitia kitengo cha Ustawi wa jamii  umemtafutia kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru Ophans Centre Mama aliyejifungua mapacha wanne na kubakia wawili baada ya kuugua Nimonia kwa ajili ya uangalizi wa karibu.

Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa Hospitali hiyo kumfuata mama mwenye watoto hao Aida Nakawala(25) pamoja na mapacha wake waliobaki kutoka kijijini kwao Chiwanda Wilaya ya Momba mkoani hapa na kuwalaza hospitalini hapo kwa uangalizi wa karibu kwa muda wa zaidi ya wiki moja.

Aidha baada ya afya za watoto hao  kuimarika kwa kiwango kikubwa pia Uongozi wa Hospitali hiyo imemtafutia hifadhi katika kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole jijini Mbeya kwa ajili ya uangalizi wa karibu kutoka kwa wauguzi na maafisa wa ustawi wa Jamii kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwakabidhi watoto hao pamoja na mama yao kwenye uongozi wa kituo cha Nuru Orphans centre, Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Aisha Mtanda, alisema wameguswa na mazingira anayoishi mama huyo na kuamua kumpa uangalizi kwa miezi sita zaidi.

Alisema jukumu hilo halipaswi kufanywa na Hospitali kwa kuwa tayari  walikuwa wamemaliza jukumu lao la kumhudumia alipokuwa ana matatizo lakini wamelazimika kubeba jukumu hilo baada ya kuguswa na mazingira na hali ya makazi ya familia hiyo.

Alisema Hospitali imekubaliana na uongozi wa Kituo cha Nuru kwamba apewe hifadhi mama huyo na watoto wake ili apate uangalizi wa karibu ikiwa na lengo la kunusuru maisha ya watoto waliobaki kutokana na wengine kupoteza maisha kiuzembe kwa ugonjwa wa Nimonia.

Aliongeza kuwa Hali ya hewa ya Mkoa wa Mbeya kwa siku zijazo kunakuwa na baridi kali sana hivyo watoto wasipokuwa kwenye uangalizi wa karibu wanaweza kupatwa na ugonjwa wa Nimonia tena kwa kukosa matunzo kama ya awali.

Kwa upande wake, Meneja wa Kituo cha Nuru, Amanda Fihavango alisema alikubali jukumu la kuwapokea watoto hao pamoja na mama yao kutokana na kuguswa na hali iliyowakuta ya kupotea kwa watoto wawili kati ya wanne.

Aliongeza kuwa ingawa anakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kiuchumi atajitahidi kwahudumia kadri ya uwezo wake na kuomba wasamaria wema watakaoguswa na jambo hilo kujitolea kwa hali na mali kufanikisha kuokoa uhai wa watoto hao pamoja na wengine anaowalea.

Alisema kituo chake hupokea watoto waliookotwa baada ya kutupwa na wazazi wao au mama zao kufariki mara baada ya kutoka kujifungua ambao hupelekwa na Serikali kupitia Ustawi wa Jamii ingawa haichangii fedha zozote baada ya kuwapeleka.

Mtu yoyote mwenye kuguswa anaweza kuwasilisha mchango wake kituoni hapo au kuwasiliana na Meneja wa Kituo cha Nuru kupitia namba za Simu  0754 043004 kwa ajili ya kusaidia watoto hao pamoja na mama yao kuishi hapo kwa muda wa miezi sita.

Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments: