LIGI ya Kombe la Bodaboda Jiji la Mbeya
inatarajia kuanza kutimua vumbi Mei 3, Mwaka huu ikizishirikisha timu za
waendesha pikipiki maarufu kwa jina la Bodaboda kwenye viwanja vya shule ya Msingi
Mwenge.
Ligi hiyo imeandaliwa na kampuni ya
Citysign Promotion and Marketing Agency yenye makao makuu jijini Mbeya
ikishirikiana na wadau mbali mbali wapenda michezo pamoja na chama cha Mpira wa
Miguu Jiji la Mbeya(MUFA).
Akizungumza kuhusu kukamilika kwa
maandalizi ya ligi hiyo, mmoja wa Viongozi wa Kampuni hiyo, Geophrey
Mwangunguru, alisema tayari timu 16 zimethibitisha kushiriki ligi hiyo baada ya
kukamilisha kujaza fomu maalumu zinazotumiwa na TFF.
Alisema timu hizo zitagawanywa katika
makundi manne ambapo kila kundi litakuwa na timu nne zitakazo chezwa mara nne
kwa wiki kutokana na kutumika kwa kiwanja kimoja cha Mwenge Shule ya
Msingi kilichopo Soweto jijini hapa.
Aidha alizitaja zawadi ambazo washindi
watajinyakulia ni kwa mshindi wa kwanza atakaeibuka na pikipiki moja mpya huku
mshindi wa pili akijipatia fedha taslimu shilingi Laki saba na mshindi wa tatu
akiondoka na shilingi Laki tatu taslimu.
Kwa upande wake Mratibu wa Ligi hiyo
kutoka kampuni ya Citysign Promotion, Charles Mwanjisi, alisema lengo la
kuandaa ligi kwa ajili ya madereva wa boda boda ni kuwakutanisha na jamii ili
kuondoa dhana potofu ya kwamba bodaboda ni wahuni pamoja na kutoa burudani.
Nao baadhi ya viongozi wa timu hizo
waliishukuru kampuni hiyo kwa kuwakumbuku na kuwathamini kama na wao ni watu
ndani ya jamii kwa kuwaandalia ligi ambayo itachangia kufahamiana miongoni mwa
jamii na madereva.
Walisema ni lazima washiriki ligi hiyo
kikamilifu ili kuwatia nguvu waandaaji ili washawishike na siku nyingi kutokana
na mwitikio watakaoupata kutoka kwa washiriki wa ligi hiyo ambao ni madereva wa
pikipiki.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment