Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi
Jeshi la
Polisi Mkoani Mbeya limewafukuza kazi Askari 6 wa kikosi cha Usalama
barabarani Wilaya za Rungwe na
Mbeya kwa tuhuma za kuomba,kushawishi na kupokea rushwa.
Kamanda wa
Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amewatataja Askari hao kuwa
ni pamoja na waliokuwa wakifanya kazi wilaya ya Mbeya barabara ya Mbeya/Tunduma
eneo la Songwe ni Copro Jonson,PC Rymond na PC Simon.
Msangi
amewataja wengine kuwa ni pamoja Sajini Hezron,PC Shaban na PC Kajolo ambao
walikuwa wanafanya kazi barabara ya Mbeya/Rungwe wilaya ya Rungwe.
Askari hao
walikuwa wanakabiliwa na makosa hayo na walifikishwa katika Mahakama ya Kijeshi
na Hukumu kutolewa Aprili 24 mwaka huu na kupewa adhabu ya kufukuzwa kazi.
Aidha
Kamanda Msangi amesema Jeshi lake halitasita kuwafukuza kazi Askari
watakaokwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi na Askari yeyote
atakayekwenda kinyume atakumbwa na adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa
kazi au kufikishwa mahakamani.
Askari
wengine waliofukuzwa kazi hivi karibuni ni pamoja na PC James Kagomba ambaye
amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa
kutumia silaha,WP Prisca Kilwai anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mtoto.
Wengine
wliohukumiwa kifungo cha mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila
kukusudia ni DC Marcelino Venance mwenye namba 8084,PC Juma Idd mwenye namba
3117 na Askari wa Mgambo MG Jackson Mwakalobo ambao walidaiwa kusababisha kifo
cha mwanafunzi Dentho Kajigili aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari
Ivumwe ya Jijini Mbeya.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment