Picha ya pamoja
Mkuu wa
Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro amewataka wakulima wa zao la Tumbaku kufanya
kazi kwa malengo ili kuboresha maisha yao na Watanzania ili kupata matokeo
makubwa sasa(BRN).
Ameyasema
hayo alipokuwa anafungua semina iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa wakulima wa
zao la Tumbaku katika Ukumbi wa Sapanjo unaomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya
ili kuleta tija kwa wakulima ambao wamekuwa na maisha duni.
Kinawiro
ameitaka Benki ya NMB kutoa mikopo nafuu kwa wakulima wa Tumbaku na kukopesha
Pembejeo kwa gharama nafuu ili vyama viweze kujikwamua kiuchumi kwa ajili ya
kupata majawabu sahihi na Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Benki
hiyo.
Aidha
amewataka viongozi wa vyama vya Ushirika na Benki kufanya kazi kwa uadilifu na
kuacha kukwepa kutorosha Tumbaku na kupeleka mikoa mingine na nchi jirani kwa
nia ya kukwepa madeni wanayodaiwa pia kufanya hivyo kunakosesha serikali mapato
yake yanayotokana na ushuru.
Pia
amewataka wakulima wa zao la Tumbaku kuweka pesa benki na kuhakikisha wanapanda
miti ili kutunza mazingira na kupata nishati mbadala ili kuhifadhi mazingira ya
Wilaya ya Chunya.
Hata hivyo
Mkuu wa wilaya ya Chunya alitumia fursa hiyo kuiomba Benki ya NMB kusaidia
mazao mengine kama ufuta ambayo yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa pato la
wilaya hiyo.
Kwa upande
wake Mwakilishi wa Meneja wa Kanda Sumka Mbuba amesema Benki ya NMB ina mkakati
wa kuwa karibu na wakulima wa mazao mbalimbali na kuendesha semina mbalimbali
zitakazowasaidia wakulima kujikwamua kiuchumi kama siku za hivi karibuni
walifanya semina ka hii kwa wakulima wa zao la Kahawa ilyojumuisha wilaya za
Mbeya,Mbozi,Rungwe,Ileje na Mbeya.
Meneja wa NMB wilaya Chunya Musa Mumba alisema Benki yake ipo tayari kutoa mikopo kwa
wakulima wa zao la Tumbaku na kuwataka kuwa waaminifu katika kurejesha mikopo
kwa wakati ili iweze kusaidia wakulima wengine.
Na Mbeya yetu
Chunya
|
No comments:
Post a Comment