Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, April 15, 2014

BONANZA! BONANZA! BONANZA! NA KABWE DUST MOTEL.

Gardner  G. Mwakasyuka Mkurugenzi wa Kabwe Dust na mwandaaji wa Bona za hilo akiongea na washiriki


Baadhi ya viongoziwa timu za Watangazaji wa Vituo vya Redio Jiji la Mbeya, Mashabiki wa Timu za Mpira wa miguu za Tanzania Prison na Mbeya City wakimsikiliza kwa makini muadaaji wa bonanza hilo


KABWE DUST MOTEL iliyopo Kabwe Jijini Mbeya imeandaa Bonanza kubwa la Pasaka litakalofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni Tarehe 19/04/2014 hadi tarehe 20/04/2014 likihusisha Mpira wa miguu.

Bonanza hilo litawashirikisha timu za Watangazaji wa Vituo vya Redio Jiji la Mbeya, Mashabiki wa Timu za Mpira wa miguu za Tanzania Prison na Mbeya City zikisindikizwa na Timu maarufu za Majiko Fc na Makunguru Fc zote za jijini Mbeya.

Bonanza hilo litapambwa na Msanii maarufu kutoka kwenye kundi la Kabwe Dust maarufu kwa jina la JAJI K anayetamba na nyimbo kali kibao kwa muda wa siku zote mbili yaani Jumamosi ya Pasaka na Jumapili ya Pasaka.

Bonanza hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL), SBC (T) Co.Ltd chini ya kinywaji chao cha Pepsi Dare for More pamoja na Mbeya Spring Water.

Mshindi wa kwanza katika Bonanza hilo litakaloendeshwa kwa mtindo wa Mtoani atanyikulia fedha taslimu shilingi Laki tano(500,000/=), Mshindi wa Pili Shilingi laki tatu(300,000/=) na mshindi wa Tatu  Shilingi laki mbili(200,000/=).

Baadhi ya timu zitakazoshiriki ni pamoja na timu ya Mashabiki wa Tanzania Prison, Mashabiki wa Timu ya Mbeya City Fc, Highland Fm, Bomba Fm, Sweet Fm, Generation Fm, Rock Fm na Mbeya Fm.

Vinywaji na vyakula mbali mbali vitapatikana uwanjani hapo, Nyote mnakaribishwa kujionea watangazaji wa Redio wanavyosakata kabumbu safi na lenye kuvutia.

No comments: