Vitendo vya ukatili wa kijinsia ni moja
ya sababu iliyochangia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Mikoa
ya Kanda ya Nyanda za juu kusini.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Kupinga
Vitendo vya ukatili wa Kijinsia wa Walter Reed Program, Thorm Chacha
wakati wa Semina kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli
ya Mbeya Peak iliyopo jijini hapa.
Alisema sababu hiyo ni kwa mujibu wa
utafiti uliofanywa na Shirika la Walter Reed Programu kwa Kushirikiana na
Shirika la Henry Jackson For Medical Research la Marekani ambao unaonesha
ukatili wa kijinsia ndani ya familia na Kaya huchangia maambukizi ya virusi vya
Ukimwi.
Chacha alibainisha kuwa utafiti
umeonesha kuwa tabia za wanaume kukwepa majukumu yao ndiyo kiini cha
tatizo ya kuongezeka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na kuchangia
kuongezeka kwa maambukizi mapya.
Alisema vitendo vya ukatili
vinavyofanywa na wanaume ni pamoja na kutelekeza familia zao hali ambayo
imesababisha watoto kutopata malezi ya wazazi wote na hivyo wanajikuta wakiwa
katika mazingira hatarishi pindi ndoa zinapovunjika na familia kusambaratika.
Alisema ipo haja kwa mashirika
yanayojishughulisha na kupinga vitendo vya ukatili nchini kuweka nguvu zaidi
maeneo ya vijijini,maeneo ambayo wanawake wameachiwa mzigo mkubwa wa kulea
familia.
Aliongeza kuwa katika kukabiliana na
ongezeko la maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi serikali na wadau pamoja na
wananchi kwa ujumla mkoani Mbeya wanapaswa kusimamia ipasavyo sheria zilizopo
dhidi ya watu wanaodaiwa kufanya ukatili wa kijinsia.
Alisema ili kuhakikisha ukatili wa
kijinsia na maambukizi ya ukimwi yanapungua shirika hilo limeanzisha vituo vya
kushughulikia ndani ya Mkoa wa Mbeya ambavyo viko katika Wilaya 6, kata 27 na
vijiji 121 pamoja na Jiji la Mbeya.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment