Mgonjwa akisubiri huduma
Dawa
zinazosambazwa na Serikali katika zahanati ya kijiji cha Malangali kata ya
Totowe wilaya ya Chunya zipo hatarini kuharibika kutokana na utunzwaji mbovu.
Muuguzi wa
kituo hicho Pilly Ntongolo amekiri kuwepo kwa tatizo hilo kwa muda mrefu tangu
zahanati hiyo kuzinduliwa kwa mbio za mwenge miaka miwili iliyopita huku
uongozi wa kijiji na kata kushindwa kuchukua hatua madhubuti.
Ntongolo
amesema kuwa dawa hizo zimekuwa zikitunzwa hovyo kutokana na kutokuwepo kwa
shelfu za mbao ambazo zingewezesha kupangwa kwa utaratibu unaoeleweka,lakini imekuwa tofauti
baada ya uongozi wa kijiji kushindwa kununua mbao za kutengenezea shelfu hizo.
Hali imekuwa
mbaya zaidi baada ya utaratibu mpya wa kusambaza dawa vijijini kupitia mpango
wa shirika la Bohari na usambazaji
dawa[MSD]kwa walengwa kuzambaza dawa katika zahanati hiyo kulundikwa
hovyo bila utaratibu hali ambayo ina hatarisha usalama wa dawa hizo.
Uchunguzi
umebaini kuwa kituo hicho chenye namba za MSD 105866 kuwa na tatizo pia na
tatizo kubwa la kuharibika dari baada ya mchwa na popo kuharibu dari na kusababisha
dawa hizo kumwagikiwa na vumbi pia na mikojo ya popo hali inayohatarisha afya
za watumiaji wa dawa hizo.
Pia zahanati
hiyo inakabiliwa na tatizo la kuwepo maji hali inayolazimu muuguzi huyo
kulazimika kuchota maji kutoka kwake wakati wa kutoa huduma ya kuzalisha kwa
wajawazito wanaofika kujifungua.
Aidha vyoo
vya zahanati hiyo vimeziba kutokana na ukosefu wa maji hali inayolazimu wagojwa
kujisaidia vichakani kutokana na kukosekana kwa maji hali inayohatarisha afya
kwa wagonjwa.
Changamoto
nyingine inayoikabili zahanati hiyo ni pamoja na mazingira machafu ambapo nyasi
zimeota hadi katika upenu wa zahanati,ambapo muuguzi hulazimika kuacha huduma
kwa wagonjwa ili kupunguza uchafu uliokithiri.
Mtendaji wa
kijiji hicho Yaledi Mwanguku hakuwa tayari kumpeleka mwandishi katika zahanati
hiyo akidai muuguzi hayupo ,lakini mwandishi alipokwenda alimkuta muuguzi hali
inayoonesha kutokuwa tayari kujibia kero hii.
Hivi sasa
zahanati hiyo haina Mwenyekiti wa Kamati ya Afya kutokana na Ahmed Ndauka
kujiuzuru kutokana na tofauti baina yake na muuguzi ambapo Kamati ya Afya ya
wilaya ilifika kutatua mgogoro huo.
NaEzekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment