Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, March 31, 2014

KIHUMBE YAZINDUA KITUO CHA VIJANA MBEYA.

 Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dk Samwel Lazalo akikata utepe kuzindua kituo cha Vijana mbeya


 Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dk Samwel Lazalo, amelipongeza shirika la Walter Reed Program(WRP) linalomilikiwa na watu wa Marekani lenye makao makuu mkoani Mbeya kwa kufadhili miradi inayowanufaisha wakazi wa jijini hapa.

Meneja wa Kihumbe, Ptolemy Samwel, alisema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni kutokana na vijana wa kike na kiume kuathirika zaidi na maambukizi ya Ukimwi na kukosekana sehemu maalumu ya kuwakutanisha na kupewa elimu.













Shirika la Kikundi cha Huduma Majumbani Mkoa wa Mbeya(KIHUMBE) limeanzisha kituo cha Vijana katika Kata ya Forest (Foresti ya zamani) Jijini Mbeya.

Meneja wa Kihumbe, Ptolemy Samwel, alisema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni kutokana na vijana wa kike na kiume kuathirika zaidi na maambukizi ya Ukimwi na kukosekana sehemu maalumu ya kuwakutanisha na kupewa elimu.

 Alisema Shirika la Kihumbe limeanzisha kituo maalumu cha vijana baada ya kuona vijana wengi jijini hawana sehemu ya kukutana na kujadili matatizo yao iliona ni muhimu kuwepo kwa kituo cha vijana ambacho pia watatumia kujadili njia mbali mbali za utekelezaji wa mkakati wa kuzuia maambukizi ya VVU/UKIMWI.

Aliongeza kuwa kutokana na ukosefu wa ajira kituo kiliamua kuwawezesha vijana kwa kuwapatia elimu ya ujasiliamali kupitia vikundi vyao vilivyopo katika Kata mbali mbali za jijini Mbeya ili kuwawezesha kujua fursa zilizopo na kuweza kuzitumia ili waweze kujiajiri wenyewe.

Alizitaja shughuli zitakazotolewa katika kituo hicho kuwa ni pamoja na kutoa elimu ya VVU/UKIMWI kwa njia za sinema, Elimu ya matumizi sahihi ya kondomu, magonjwa ya ngono, mtandao wa ngono, ngono mtambaluka na ugawaji wa kondomu.

Aliongeza kuwa shughuli zingine zitakuwa ni kutoa huduma za ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya ukimwi kwa hiari, huduma ya daktari, michezo mbali mbali ya ndani ya kituo na nje, elimu ya ujasiliamali pamoja na Msaada wa masomo kwa njia ya mtandao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dk Samwel Lazalo, amelipongeza shirika la Walter Reed Program(WRP) linalomilikiwa na watu wa Marekani lenye makao makuu mkoani Mbeya kwa kufadhili miradi inayowanufaisha wakazi wa jijini hapa.

Pongezi hizo alizitoa alipokuwa akizindua kituo cha vijana kinachomilikiwa na kikundi cha Huduma majumbani Mkoa wa Mbeya(KIHUMBE) kilichojengwa chini ya ufadhili wa Shirika la WRP  kilichopo Forest ya Zamani jijini hapa.

Alisema  msaada wa ujenzi huo utawanufaisha zaidi vijana wengi wa Jiji la Mbeya na wageni watakao tembelea kwa kufundishwa maarifa mbali mbali pamoja na elimu juu ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Alitoa wito kwa vijana na wamiliki wa kituo hicho kuhakikisha wanatumia kama ilivyokusudiwa ili kuwafurahisha walipa kodi wa Marekani ambao ndiyo waliotoa ufadhili kupitia shirika lao la WRP kwa vijana kutumia kupata maarifa mbali mbali yatakayowasaidia katika maisha.

Mkurugenzi huyo aliongeza kwa kuwataka Viongozi wa Serikali katika ngazi ya kata na Jiji sehemu kilipojengwa kituo hicho kuhakikisha wanaunga mkono jitihada za KIHUMBE na WRP ili kupata malengo yanayotarajiwa kutokana na kituo hicho.

Na Mbeya yetu






No comments: