Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, February 12, 2014

SAKATA la Wafanyabiashara kufunga maduka yao wakigomea Mashine za kielektroniki za kutolea Stakabadhi zilizopendekezwa na Serikali maarufu kwa jina la EFDs limezidi kushika kasi baada ya wafanyabiashara ya Wilaya ya Kyela na Soko la Sido Jijini Mbeya nao kufunga biashara zao.
SAKATA la Wafanyabiashara kufunga maduka yao wakigomea Mashine za kielektroniki za kutolea Stakabadhi zilizopendekezwa na Serikali maarufu kwa jina la EFDs limezidi kushika kasi baada ya wafanyabiashara ya Wilaya ya Kyela na Soko la Sido Jijini Mbeya nao kufunga biashara zao.

Zoezi la wafanyabiashara hao kufunga maduka hayo lilianza juzi na jana katika Wilaya ya Kyela na Jiji la Mbeya ikiwa ni muda mfupi baada ya Polisi kulazimika kutumia Mabomu ya machozi kuwatuliza wafanyabiashara wa Soko la Mwanjelwa walipogomea mashine hizo Mwishoni mwa mwaka jana.

Hata hivyo baadhi ya Wafanyabiashara wamesema wao wanachogomea ni bei za Mashine hizo kuwa ni kubwa na haziendani na mitaji ya biashara zao ambapo waliitaka Serikali ama kupunguza bei hizo ambazo wanalazimishwa kununua kwa shilingi Laki saba hadi Laki nane au kuwakopesha ili wawakate kwenye kodi humo humo.

Walisema suala la mashine hizo linaonekana kama ni miradi ya watu wachache hali inayowayumbisha wafanyabiashara na kuwanyika haki yao ya msingi ingawa wanatambua umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya Nchi lakini siyo kwa kuwalazimisha kununua kwa bei kubwa.

Aidha walisema ni vema TRA wakatumia mashine hizo kama ilivyo Idara za Maji na Tanesco wanapomfungia mteja wake Mita inakuwa bado ni mali ya Shirika hivyo na wao wangezigawa bure kwa Wafanyabiashara ili waendelee kukusanya ushuru na siyo kuwalazimisha kuwauzia kitu ambacho hawana faida nacho.

Hata hivyo zoezi hilo la kufunga maduka limeonekana kuwa na athari kubwa kutokana na baadhi ya Wafanyabiashara wadogo wasiostahili kuwa na mashine hizo kulazimishwa kufunga maduka yao na wafanyabiashara wakubwa wanaogomea hali inayowaathiri na wao.

Na Mbeya yetu

No comments: