Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, February 12, 2014

SERIKALI imetakiwa kuondoa mfumo wa Elimu ya Siasa katika Shule za Msingi na Sekondari na kuingiza somo la Biashara na kupewa kipaumbele kwa ajili ya Maendeleo katika kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Nchi kwa ujumla.

Makamu Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mbeya, Graciano Kunzugala wakati akitoa mafunzo kwa wanachama wa Chama cha Vijana Wanawake Wakristu Tanzania(YWCA) Tawi la Mbeya yanayofanyika katika ukumbi wa Asasi ya Elimisha uliopo Ilomba Jijini Mbeya.

Mratibu wa YWCA Mkoa wa Mbeya, Thabita Bugali, alisema semina hiyo itaendeshwa kwa muda wa siku mbili ikiwa ni mfululizo wa kuwapatia wanachama mafunzo yatakayoinua asasi ili iweze kupata mafanikio chanya katika jamii ikiwa ni pamoja na kusaidia kutatua changamoto mbali mbali zinazoizunguka jamii.

 Mwandishi wa Habari, Festo Sikagonamo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Elimisha ambao pia wamefadhili ukumbi alisema suala la usafi na utunzaji wa mazingira linaanza na mtu mwenyewe ndani ya kaya yake.


 Chama cha Vijana Wanawake Wakristu Tanzania(YWCA) Tawi la Mbeya wakiwa makini kuwasikiliza wawezeshaji




SERIKALI imetakiwa kuondoa mfumo wa Elimu ya Siasa katika Shule za Msingi na Sekondari na kuingiza somo la Biashara na kupewa kipaumbele kwa ajili ya Maendeleo katika kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Nchi kwa ujumla.

Aidha imeelezwa kuwa somo hilo linapaswa kupatikana katika ngazi ya chuo kikuu pekee ili kuweka mipaka ya kiutendaji kuwa na utofauti baina ya Wanasiasa na wataalamu kutoingiza Siasa katika shughuli za maendeleo zinazosababisha kukwama kwa vitu vingi vinavyosababishwa na viongozi wa Siasa kuingilia kazi ambazo hawana utalaamu nazo.

Hayo yalibainishwa na Makamu Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mbeya, Graciano Kunzugala wakati akitoa mafunzo kwa wanachama wa Chama cha Vijana Wanawake Wakristu Tanzania(YWCA) Tawi la Mbeya yanayofanyika katika ukumbi wa Asasi ya Elimisha uliopo Ilomba Jijini Mbeya.

Kunzugala alisema utaratibu wa kufundisha Siasa kuanzia ngazi ya chini badala ya biashara umesababisha viongozi wa Kitaifa kuhubiri zaidi habari ya Umoja Mshikamano na amani bila kugusia suala la kukua kwa uchumi na fursa za biashara kwa lengo la kukuza kipato cha nchi na Mtanzania mmoja mmoja.

Alisema hivi sasa Siasa imeingia katika utendaji hali inayosababisha watu kushindwa kuzungumzia njia mbadala za kumuinua na kumwezesha mwananchi mwenyekipato cha chini kuongeza kipato chake ambapo pia amani umoja na mshikamano utapatikana kutokana na kuwa na uchumi mzuri.

Kwa upande wake Mratibu wa YWCA Mkoa wa Mbeya, Thabita Bugali, alisema semina hiyo itaendeshwa kwa muda wa siku mbili ikiwa ni mfululizo wa kuwapatia wanachama mafunzo yatakayoinua asasi ili iweze kupata mafanikio chanya katika jamii ikiwa ni pamoja na kusaidia kutatua changamoto mbali mbali zinazoizunguka jamii.

Alisema chama hicho kimepewa mafunzo hayo kwa ufadhili wa The Faundation for Civil Society,ambapo watapata fursa ya kujifunza namna ya kuandaa mpango mkakati, uhifadhi wa misitu na vyanzo vya maji pamoja na Mazingira na usafi wa mazingira kwa ujumla wake.

Naye mwezeshaji katika mafunzo hayo ambaye ni mwanamazingira na Mwandishi wa Habari, Festo Sikagonamo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Elimisha ambao pia wamefadhili ukumbi alisema suala la usafi na utunzaji wa mazingira linaanza na mtu mwenyewe ndani ya kaya yake.

Alisema ili kuondokana na kero ya uchafu na uharibifu wa mazingira katika jiji la Mbeya ni vema kila Mwananchi akapata fursa ya kueleweshwa juu ya namna ya utunzaji wa mazingira kwa kuzingatia usafi pamoja na vyanzo vya maji kwa kutokata miti ovyo.

Alisema endapo Mazingira yakawa masafi kwa wananchi kuleweshwa kutupa taka katika maeneo yaliyoruhusiwa na kuzolewa kwa wakati itachangia kuongeza pato la Halmashauri ya Jiji kutokana na Wageni wengi kuvutiwa na mazingira hali itakayosababisha kukua kwa uwekezaji.

Aliongeza kuwa madhara ya uchafu wa mazingira na uharibifu wa mazingira ni makubwa sana kwa sababu yanaathiri pia uchumi wa Nchi na mtu binafsi ambapo kutokana na uchafu wa mazingira mtu anaweza kupata magonjwa hivyo badala ya kufanya kazi ya uzalishaji atalazimika kwenda Hospitali kutibiwa magonjwa yatokanayo na uchafu.

Na Mbeya yetu



No comments: