Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, February 11, 2014

JESHI LA MAGEREZA KUZINDUA "DUTY FREE SHOP" - RUANDA, MBEYA


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Mbarak Abdulwakil anatarajia kuzindua rasmi Magereza "Duty Free Shop" - Ruanda, Mbeya kesho saa 3:30 asbuhi Februari 12, 2014 katika Viwanja vya Ofisi ya Magereza Mkoa wa Mbeya ambapo shughuli hiyo itashuhudiwa na Viongozi mbalimbali toka Ofisi za Serikali, Binafsi pamoja na Wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya Gereza Kuu Ruanda, Mbeya.

Mpango huu wa ujenzi wa Magereza "Duty Free Shops" katika Mikoa ya Kimagereza Kiutawala unatekelezwa  kwa Mafanikio makubwa na Uongozi wa Jeshi la Magereza unaosimamiwa kimkakati na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja hivyo kutimiza adhima  ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye manufaa  Maafisa, Askari wa Jeshi la Magereza pamoja na familia zao katika maeneo yao ya kazi.

Aidha, mpaka sasa jumla ya "Duty Free Shops" tano (05) zimezinduliwa sehemu mbalimbali hapa nchini hususani katika Mikoa ya Dar es Salaam(Ukonga), Dodoma(Gereza Isanga), Morogoro(Chuo cha Ufundi na Udereva Kingolwira), Kilimanjaro(Gereza Karanga, Moshi) na Mwanza(Gereza Butimba).

Kuzinduliwa kwa Magereza "Duty Free Shop" - Ruanda, Mbeya kunafanya idadi yake kuongezeka na kufikia jumla ya Magereza "Duty Free Shop" sita(06) ambazo zimekamilika hapa Nchini katika Mikoa ya Kimagereza Kiutawala.

Vyombo vya Habari ikiwa wadau muhimu katika dhima ya kuuhabarisha umma vinakaribishwa kwenye tukio la uzinduzi rasmi wa Magereza "Duty Free Shop" - Ruanda, Mbeya kesho Februari 12, 2014 kuanzia saa 3:30 asbuhi katika Viwanja vya Ofisi za Magereza Mkoa wa Mbeya.

Imetolewa na;

Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Mbeya
Februari 11, 2014.


No comments: