Katika hali isiyokuwa ya Kawaida Shirika
la Nyumba la Taifa(NHC) Mkoa Mbeya limemfungia mpangaji wake ndani ya duka
katika kile kilichodaiwa kuchelewa kulipia pango la chumba hicho kwa muda
uliokusudiwa ambao ni Mwanzo wa Mwezi.
Tukio hilo ambalo lilivuta hisia za Watu
wengi kutokana na afya ya Mpangaji huyo anayesumbuliwa na Kisukari kwa Muda
mrefu limetokea Leo majira ya saa nne kati kati ya Jiji la Mbeya ambapo
Watumishi wa Shirika hilo walifunga Duka la Kuuzia vifaa vya Maofisini(Stationary)
inayojulikana kwa jila la Rubi iliyopo Posta.
Akizungumzia Dirishani kufuatia
kufungiwa kwa duka lake na yeye akiwa ndani pamoja na wafanyakazi wake wawili,
Mmiliki wa Duka hilo, Boniface Ishabakaki, alisema ameshangaa kufanyika kwa kitendo
hicho kwa sababu tayari Mke wake alikuwa ameshaongea na Meneja na kumtumia
Fedha kwa njia ya Mpesa tangu saa nne lakini alivyowaeleza walishindwa
kumuelewa.
Hata hivyo baadhi ya watu walioshuhudia
kitendo hicho wamelaani vikali kwa kile walichodai Shirika hilo limegeuka adui
wa wapangaji wao ambao hata hivyo hawana madeni ya kutisha na siyo wasumbufu
kwenye ulipaji na kuongeza kuwa mzee huyo amekuwa mpangaji wa shirika hilo
tangu Mwaka 2000.
Walisema kitendo cha kumfungia mtu
dukani au chumbani ni hatari kutokana na majanga ya moto kuibuka pasip taarifa
hivyo kama mtu yuko ndani na majanga yametokea ni vipi wanaweza kumuokoa ili
hali amefungiwa nje na kuongeza kuwa mgonjwa wa kisukari kawaida anahitaji
kwenda katika haja ndogo kila mara.
Aidha kutokana na kelele za baadhi ya
waandishi waliofika katika hilo na kulazimu kupiga Simu Polisi ambapo muda
mfupi baadaye alionekana mmoja wa wafanyakazi wa Shirika hilo ambaye hakutaka
kuzungumzia ishu yoyote alijitokeza na kufungua Duka hilo na kutokomea.
Kwa upande wakeKaimu Meneja wa shirika la Nyumba mkoa wa Mbeya S.C Katanga amesema Ndugu Ishabakaki ni mpangaji wao wa nyumba Na. 003 Kiwanja Na. 6/3 Mtaa wa Lupaway. Mbali na jitihada zote za kumdai kodi amekuwa msumbufu kulipa pia historia yake ya ulipaji kodi si mzuri hata kulifikisha shirika katika hatua ya kutoa Notisi na wakati mwingine kumpeleka Dalali.
Aidha kwa mwezi January 2014 Ishabakaki alipewa Demand Note iliyomtaka alipe kodi yake yote ya Tsh 222,450, ndani ya juma la kwanza la mwezi na hakutekeleza wajibu wakehuo.
Shirika liliendelea kumkumbusha ambapo tarehe 18, 22, na 27 alitembelewa na maafisa wa shirika kumkumbusha na bado akashindwa kutekeleza wajibu huo.
Mnamo tatehe 29/01/2014 shirika liliamua kufunga sehemu ya Ishabakaki kwa muda ili kumhamasisha alipe deni na kweli baada ya kufungiwa alilipa deni hilo lote la Tsh 222,450.00
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment