Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, January 30, 2014

MUUNGANO wa Jamii Tanzania(MUJATA) umeingilia kati sakata la upotevu wa Mtoto wa Miaka mitano uliotokea Wiki iliyopita katika Mtaa ya Ghana Mashariki kata ya Ghana Jijini Mbeya na kuwaagiza waliohusika na kitendo hicho kumrudisha mtoto huyo ndani ya siku tatu.

 Steven Uswege(5) alipotea Januari 17, Mwaka huu majira ya saa Tano asubuhi baada ya kwenda dukani kununua pipi akiwa na mwenzie ambapo yeye hakuweza kurudi hadi sasa.

Mwenyekiti wa Mujata,Chifu Soja Shayo Masoko, alipokuwa akizungumza na mamia ya wakazi wa Mtaa wa Ghana waliokuwa wamefurika kujua hatma ya upotevu wa Mtoto baada ya Kamati iliyokuwa imeundwa na Serikali ya Mtaa kuomba msaada kwa Mujata baada ya wao kutafuta bila mafanikio kwa zaidi ya siku kumi.

Mwenyekiti wa wa Mtaa wa Ghana Mashariki, Philimon Mwansasu, alisema walilazimika kuomba msaada toka mujata kutokana na mafanikio yalioneshwa na jamii hiyo katika maeneo mbalimbali kufanikisha kuibua mambo mengi yaliyojitokeza katika jamii yakiwemo ya upotevu wa watoto.






Wazazi wa mtoto aliyepotea

Add caption



MUUNGANO wa Jamii Tanzania(MUJATA) umeingilia kati sakata la upotevu wa Mtoto wa Miaka mitano uliotokea Wiki iliyopita katika Mtaa ya Ghana Mashariki kata ya Ghana Jijini Mbeya na kuwaagiza waliohusika na kitendo hicho kumrudisha mtoto huyo ndani ya siku tatu.

Agizo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa Mujata,Chifu Soja Shayo Masoko, alipokuwa akizungumza na mamia ya wakazi wa Mtaa wa Ghana waliokuwa wamefurika kujua hatma ya upotevu wa Mtoto baada ya Kamati iliyokuwa imeundwa na Serikali ya Mtaa kuomba msaada kwa Mujata baada ya wao kutafuta bila mafanikio kwa zaidi ya siku kumi.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mjumbe wa Kamati ya kufanikisha kupatikana kwa Mtoto, Sam Mwashula alisema Mtoto aliyefahamika kwa jina la Steven Uswege(5) alipotea Januari 17, Mwaka huu majira ya saa Tano asubuhi baada ya kwenda dukani kununua pipi akiwa na mwenzie ambapo yeye hakuweza kurudi hadi sasa.

Alisema juhudi za kutafuta zilianza mara moja ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kituo cha polisi pamoja na vikao vya mara kwa mara baina ya Wananchi na Serikali ya Mtaa ili kupeana mbinu mbali mbali za kufanikisha zoezi hilo lakini hadi Siku kumi zinafika hakuna dalili hali iliyowalazimu kuomba msaada katika Muungano wa Jamii(MUJATA).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa Mtaa wa Ghana Mashariki, Philimon Mwansasu, alisema walilazimika kuomba msaada toka mujata kutokana na mafanikio yalioneshwa na jamii hiyo katika maeneo mbalimbali kufanikisha kuibua mambo mengi yaliyojitokeza katika jamii yakiwemo ya upotevu wa watoto.

Alisema pia kitendo hicho kimetokana na baadhi ya maoni ya wananchi yaliyotokana na mikutano mbali mbali iliyofanyika mtaani hapo yenye malengo ya kuhakikisha mtoto anapatikana akiwa mzima ama mfu, ambapo mawazo ya wananchi wengi walielekeza nguvu zao kwa Mujata.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Mujata, Chifu Soja, alisema wananchi wanatakiwa kuepukana na imani za kishirikina na kuamini kwamba mtoto huyo amepotea katika mazingira hayo bali waamini kuwa alipokuwa ametoka nyumbani alishindwa kurudi nyumbani hivyo amepotea katika mazingira ya kawaida.

Aidha aliwaomba wananchi kuwa na subira kwa kile alichosema Muungano wa Jamii umeanza kulifanyia kazi suala hilo tangu walipopata taarifa ambapo Wajumbe wa Mujata wametawanyika katika Wilaya zote pamoja na mikoa jirani kuhakikisha mtoto anapatikana kwa wakati ama akiwa mzima au mfu.

Alisema anatoa siku tatu kwa mtu yoyote aliyehusika na upotevu wa mtoto huyo kuhakikisha anamrudisha ndani ya siku tatu la sivyo kitu kibaya kitamkuta ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wataalamu wa tiba asili, waganga wa kienyeji na wataalamu mbali mbali wakiwemo Machifu kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya ambao watafanya tambiko kubwa katika mtaa huo.

Hata hivyo Chifu huyo aliinua imani za watu baada ya kumuagiza Mama mzazi wa Mtoto aliyepotea Jesca Stephano kwenda kununua pipi kama aliyokuwa amenunua mtoto wake katika duka lilelile na kuichukua kwa madai kuwa itamuongoza katika kumpata mtoto.

Na Mbeya yetu

1 comment:

Anonymous said...

POLENI WANA GHANA WOTE