CHAMA cha Mapinduzi(CCM) kimesema
kinajivunia msingi uliojiwekea wa kukua kwa uchumi tangu kuzaliwa kwa chama
hicho Mwaka 1977, ambapo matokeo na matunda yake yataanza kuonekana hivi sasa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa
Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye, alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika Ofisi za Chama hicho Mkoa
wa Mbeya kuhusiana na Sherehe za kuadhimisha miaka 37 tangu kuzaliwa kwa chama
zitakazofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya.
Nape alisema katika maadhimisho ya
kuzaliwa kwa CCM, Wanavijivunia mafanikio mengi ikiwemo msingi uliojengwa wa
kukua kwa uchumi wa Nchi ambapo matokeo yake yataanza kuonekana hivi karibuni
kwa Watanzania kufaidi matunda yaliwekwa na Chama tawala.
Aidha aliwataka Watanzania na Wakazi wa
Mkoa wa Mbeya kujitokeza kwa wingi kumlaki Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na mgeni
rasmi katika maadhimisho hayo ambayo yatatanguliwa na Matembezi ya mshikamano.
Katibu huyo aliongeza kuwa Maadhimisho
ya Miaka 37 tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi huadhimishwa kila Tarehe 5
ya kila Mwaka lakini mwaka huu sherehe hizo zimerudishwa nyuma na kufanyika
Februari 2, Mwaka huu kwa kile alichodai ni kupisha siku za kazi ili wananchi
wajikite katika shughuli za uzalishaji mali.
Alisema Viongozi wa Kitaifa wameshaanza
kuwasili ambapo Katibu Mkuu wa Chama hicho atawahi kufika akifuatiwa na Makamu
Mwenyekiti wa CCM Taifa bara kabla ya kumpokea Raisi Februari Mosi tayari kwa
Sherehe za Tarehe 2 Februari Mwaka huu.
Alisema kabla ya Sherehe viongozi wa
Chama kitafanya shughuli mbali mbali za maendeleo ambazo ni kushiriki kazi za
kijamii kama ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa zahanati, usafi wa
Mazingira pamoja na kupanda miti kwenye vyanzo vya maji ndani ya Jiji la Mbeya.
Nape aliongeza kuwa Sherehe hizo
zilifunguliwa rasmi Januari 26, Mwaka huu na Makamu Mwenyekiti wa CCM Visiwani
ambaye pia ni Raisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Mahamed Shein kisha
kusherekewa katika kila ngazi kuanzia vitongoji, vijiji, Wilaya n Mikoa Nchi
nzima.
Alisema katika sherehe hizo ambazo
zitaanza na matembezi ya Mshikamano yatakayoongozwa na Mheshimiwa Raisi kuanzia
,majira ya saa Mbili asubuhi yatakayoanzia Soweto na Kuishia makao makuu ya
Ofisi za chama Mkoa na baadaye kuendelea na Sherehe katika Uwanja wa Sokoine
kuanzia majira ya saa nane mchana zikipambwa na burudani mbali mbali
zikiongozwa na Bendi ya TOT.
Na Mbeya yetu
|
1 comment:
TUMEFANIKIWA KUONDOA DIVISHENI ZIRO NA SASA TUNA DIVISHENI TANO, VERY GOOD CCM.
Post a Comment