WADAU wa sekta ya Afya nchini wametakiwa
kuwajali na kuwathamini wakunga wa Jadi kwa kuwa wamekuwa wakombozi kwa wazazi
waishio mbali na vituo vya afya pindi wanapohitaji huduma ya kujifungua.
Mwito huo ulitolewa na Mkunga wa Jadi,
Dotea Mwanakulya (60) Mkazi wa kijiji cha Magamba Wilayani Chunya alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea nyumbani kwake kujua
changamoto anazokabiliana nazo.
Mkunga huyo wa alisema anakabiliwa na
changamoto za ukosefu wa vifaa vya kujifungulia kama kitanda,godoro,mipira ya
kuvaa mikononi ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa ambapo wagonjwa wengine hufika
hapo wakiwa hawana vifaa hivyo.
Hata hivyo mkunga huyo amewaomba wadau
mbali mbali kumsaidia kupata daftari ya kutunza kumbukumbu za watoto
wanaozaliwa nyumbani kwake kwa kile alichodai kuwa hana kumbukumbu sahihi za
idadi hali ya watoto waliozaliwa kwake.
Mkunga huyo alilazimika kutoa kauli hizo
kufuatia kuwepo kwa Mwanamke mmoja kujifunga watoto mapacha mfululizo kwa
Mkunga huyo na watoto wake wakiendelea kukua vizuri.
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la
Paskalia Adrofu (37)mkazi wa kijiji cha Magamba kata ya Magamba wilaya ya
Chunya Mkoani Mbeya,alijifungua salama watoto watatu hivi karibuni kwa mkunga
wa Jadi huyo.
Paskalia amejifungua watoto wawili jinsi
ya kiume na mmoja wa kike ambapo amesaidiwa na mkunga wa jadi Dotea
Mwanakulya (60)anayeishi kijiji cha Magamba.
Paskalia alisema kwamba mume wake
aitwaye Richard Saba (55) ni mkulima hivyo imekuwa vigumu kwake kumudu gharama
za matunzo kwa watoto hao ambapo ana jumla ya watoto wanane,wakiwemo mapacha
ambao wamemaliza shule ya msingi na hawajachaguliwa kuendelea na masomo ya
sekondari.
Mama huyo alianza kujifungua mtoto wa
kwanza mwaka 1995,wa pili ambao ni mapacha mwaka 1998 wa tatu mwaka 2006,wa nne
mwaka 2009 na wa tano ambao wamezaliwa watatu amejifungua mwanzoni mwa mwaka
huu ambao wana afya njema.
Hata hivyo Paskalia alisema uongozi wa
kata akiwemo Diwani wa kata ya Magamba Chakupewa Kapalala wamefika kumtembelea
na kumjulia hali yake na kumhimiza kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili
kufuatilia afya za watoto.
Aidha mkazi mmoja wa kijiji hicho
aitwaye Luhende Luhaga ametoa ng’ombe wawili wa maziwa ili mama huyo amudu
kuwanyonyesha watoto hao bila shida kutokana na kulemewa na watoto hao.
Watoto wawili wa mwanzo wamezaliwa na
uzito wa kilo 2.8 na wa tatu amezaliwa na uzito wa kilo 2.0 ambapo Paskalia
alisema kuwa watapofikia uzito wa kilo 3 ndipo watapatiwa chanjo katika
zahanati ya Magamba.
Baadhi ya changamoto anazokabiliwa nazo
ni pamoja na nguo za watoto,chupa za kunyonyeshea,sabuni,mafuta na chupa za
chai kwa ajili ya kuhifadhia maziwa ya watoto.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment