Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, January 23, 2014

HATIMAYE ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WANNE AFIKISHWA KIJIJINI KWAO.

Sasa tunaingia kijijini kwao Chiwanda 


Tupo kijijini kwao Chiwanda na kupokelewa na mamia ya wakazi wa hapo.

Mama wanne akishuka katika gari kijijini kwao

Baba mzazi wa watoto mapacha wanne akiwa amefurahi kumpokea mkewe huku akiwa amembeba moja ya mapacha na kusema huyu ataitwa Joseph wa Mbeya yetu

Ni furaha ilioje kijijini hapo tulipokwewa vizuri sana

Mtoto Claud akimpokea mama yake mzazi kwa furaha ya kupata wadogo zake wanne yaani wee acha tu


Yaani kila mwana kijiji alitamani kuwashika watoto hao angalau apate baraka maana wakazi wa hapo wanasema neema imeingia kijijini kwao




Hii ndiyo nyumba ya wazazi wa watoto mapacha wanne 

Ndani ya nyumba hiyo na ndiyo chakula chetu kitamu kinapikwa humu tulikula msosi wa nguvu wali wa kuku na zawadi ya maembe tukapewa mungu awabariki sana wanakijiji cha Chiwanda


Hii ni nyumba mpya ambayo imejengwa kwa siku chache tu kwa ajaani wamezindua nyumba yao mpyaili ya mapokezi ya watoto mapacha wanne pesa kiasi walichotoa wasamaria wema baba mzazi wa watoto mapacha akaamua kununua bati na kuezeka nyumba hiyo yao na ndimo walipofikia mapacha hao 

 Mwenyekiti wa Kijiji cha Chiwanda, Ignas Sinkara mwenye shati la kitenge aliwapongeza waandishi hao kwa moyo walioonesha na kuwaomba kuendelea kujitolea hivyo hivyo katika majukumu mengine.


Joseph Mwaisango ambaye ni mmoja wa wakurugenzi  wa mtandao wa kijamii wa Mbeya yetu Blog







Picha ya pamoja kabla ya kuondoka kijijini hapo




Mwanamke Aida Nakawala(25) aliyejifungua watoto wanne kwa mkupuo  usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Wazazi ya Meta kwa ajili ya hifadhi ya chumba cha joto kwa watoto na huduma muhimu kwa mzazi amewasili kijijini kwao Chiwanda na kupokelewa na mamia ya wakazi wa hapo.

Mapokezi hayo yaliyofanyika jana, mara baada ya kuwasili nyumbani kwake kijijini hapo akitokea katika Hospitali ya Wazazi ya Meta alikokuwa akipatiwa matibabu, ambapo Wakazi hao walionekana kushangazwa na kitendo cha mama huyo kujifungua watoto wanne kwa mkupuo tena kwa njia ya kawaida.

Baadhi ya majirani waliokuwepo Nyumbani kwa Mwanamke huyo wakiongozwa na Serikali ya Kijiji, walisema wapo tayari kumpa msaada mama huyo shujaa wa hali na mali.

Hata hivyo wakati Wananchi wakionesha furaha na mishangao Serikali ya Kijiji pia imejipanga kuhakikisha inaisaidia Familia hiyo  ambayo haina uwezo kimaisha kutokana na baba wa Familia Webson Simkanga(28) kutegemea kilimo cha Mahindi huku akiwa na jumla ya  watoto Sita, kutunza watoto hao kwa kupanga mikakati mbali mbali ya muda mfupi na muda mrefu.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofanikisha Safari ya Mama huyo kutoka Hospitali ya Wazazi Meta hadi kijijini kwao umbali wa Kilomita zaidi ya 130, Mwenyekiti wa Kijiji cha Chiwanda, Ignas Sinkara aliwapongeza waandishi hao kwa moyo walioonesha na kuwaomba kuendelea kujitolea hivyo hivyo katika majukumu mengine.

Alisema moja ya michango iliyopatikana imesaidia huduma za mama alipokuwa Hospitali, kukarabati Nyumba atakayoishi baada ya kujifungua pamoja na kusaidia shughuli za Shamba kutokana na wazazi wote wawili kutakiwa kusaidiana katika kuwahudumia watoto hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mpumpi anapotokea Mama huyo, Winstoni Mtali, alisema mbali na juhudi zilizopangwa na serikali ya kijiji pamoja na wasamaria wema walionesha kuguswa na mama huyo tangu alipojifungua bado misaada zaidi inahitajika kutokana na mzigo huo kuwa mkubwa kwa Wanakijiji.

Alisema bado mazingira ya nyumbani kwa mwanamke huyo na kijiji kwa ujumla siyo rafiki kwa malezi ya watoto hao kutokana na nyumba yao kutokuwa katika mazingira mazuri hivyo kuhitajika michango ya hali na mali kwa ajili ya ukarabati wa nyumba hiyo ambayo inahitaji kusakafiwa, kupigwa dali, madirisha na kusakafia kuta ili watoto wasidhurike na vumbi la ndani

Waandishi waliojitolea kufanikisha safari ya Mwanamke huyo hadi kijijini kwao ni pamoja na Venance Matinya(JamboLeo), Ezekiel Kamanga(Bomba Fm Redio), Joseph Mwaisango ambaye ni mmoja wa wakurugenzi  wa mtandao wa kijamii wa Mbeya yetu Blog na Jacob Mwaisango aliyejitolea gari lake. 

Namba ya mama wanne yaani mapacha wanne ni
0769 12 51 88
au 
mwenyekiti wa kijiji
0783 87 59 99

Na Mbeya yetu
        

4 comments:

Anonymous said...

KAZI NZURI

Anonymous said...

NAWAPONGEZA SANA MBEYA YETU KWA MLICHOMFANYIA HUYU MAMA MUNGU ATAWABARIKI

Madame B said...

Mpaka namaliza kuisoma hii habari machozi ya furaha yamenitoka.
Mungu ambariki mama wanne pamoja na wote mliofanikisha mpaka pale alikofikia.
Naahidi kusafiri kuja Mbeya kumuona mama wanne.
Baba wanne.....hongera, sasa naamini utawekeza zaidi kwenye elimu za wanao.
Naahidi kuja kuwatembelea.

Anonymous said...

JAMBO JEMA SANA