Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, January 23, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Bashiru S. Madodi
 Katibu siasa na uenezi mkoa wa Mbeya.


Chama cha mapinduzi  kitafanya sherehe za kutimiza miaka 37 toka kuanzishwa kwake tarehe 05.02. 1977, sherehe hizi kwa mwaka 2014 zitafanyika katika mkoa wetu wa Mbeya tarehe 02.02.2014.

 Ifuatayo ni taarifa ya shughuli zitakazofanyika katika kufanikisha sherehe hizi.

 Tarehe 25 – 26 January  2014 maafisa wawili kutoka makao makuu watawasili katika mkoa wa Mbeya.

 Tarehe 28 january 2014, katibu wa NEC siasa na uenezi ndugu Nape Moses Nnauye atawasili katika mkoa wa Mbeya.

 Tarehe 30. 01. 2014 makamu mwenyekiti bara ndugu Philip Mangula, pamoja na sekretarieti ya taifa watawasili katika mkoa wa Mbeya.

Tarehe 31, 01, 2014 saa 4:00 hadi saa 7:00 mchana makamu mwenyekiti bara Ndugu Philip Mangula pamoja na wajumbe wa sekretarieti ya taifa watafanya ziara katika wilaya ya Mbeya mjini ili kuangalia uhai wa chama katika matawi na utekelezaji wa ilani ya uchagizi wa CCM, pia watashiriki shughuli za ujenzi wa taifa.

 Tarehe 31, 01 2014 saa 8:00 hadi 12:00 jioni, katibu mkuu wa CCM ndugu  Abdulrahman Kinana atakutana na vijana wajasiliamali wa bodaboda na bajaji.

 Tarehe  01,02, 2014 mwenyekiti wa CCM taifa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya mrisho kikwete atawasili katika mkoa wetu wa Mbeya, na tutampokea kwenye uwanja wa Ndege wa Songwe.

 Tarehe 01,02,2014 saa 08:00 mchana hadi saa 12:00 jioni katibu mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana  atakutana na wana CCM kutoka vyuo vikuu vilivyoko katika mkoa wa MBEYA.

 Tarehe 02,02,2014 saa 12:00 alfajiri mpaka saa 02 kamili asubuhi yatafanyika  matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na mwenyekiti wa CCM taifa ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, matembezi hayo yatakayoanzia Soweto na kupita mwanjelwa, sinde  yataishia ofisi kuu ya CCM mkoa wa Mbeya.

 Tarehe 02,02,2014 saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni sherehe za miaka 37 ya CCM zitakazofanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

 Tarehe 03, 02, 2014 viongozi  kuanza kuondoka katika mkoa wa Mbeya.


Imetolewa na:

Bashiru S. Madodi

Katibu siasa na uenezi mkoa wa Mbeya.

No comments: