Picha ya pamoja kabla ya kuondoka kijijini hapo
Mwanamke Aida Nakawala(25) aliyejifungua
watoto wanne kwa mkupuo usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika
Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Wazazi ya
Meta kwa ajili ya hifadhi ya chumba cha joto kwa watoto na huduma muhimu kwa
mzazi amewasili kijijini kwao Chiwanda na kupokelewa na mamia ya wakazi wa
hapo.
Mapokezi hayo yaliyofanyika jana, mara
baada ya kuwasili nyumbani kwake kijijini hapo akitokea katika Hospitali ya
Wazazi ya Meta alikokuwa akipatiwa matibabu, ambapo Wakazi hao walionekana
kushangazwa na kitendo cha mama huyo kujifungua watoto wanne kwa mkupuo tena
kwa njia ya kawaida.
Baadhi ya majirani waliokuwepo Nyumbani
kwa Mwanamke huyo wakiongozwa na Serikali ya Kijiji, walisema wapo tayari kumpa
msaada mama huyo shujaa wa hali na mali.
Hata hivyo wakati Wananchi wakionesha
furaha na mishangao Serikali ya Kijiji pia imejipanga kuhakikisha inaisaidia
Familia hiyo ambayo haina uwezo kimaisha kutokana na baba wa Familia
Webson Simkanga(28) kutegemea kilimo cha Mahindi huku akiwa na jumla ya
watoto Sita, kutunza watoto hao kwa kupanga mikakati mbali mbali ya muda
mfupi na muda mrefu.
Akizungumza na waandishi wa habari
waliofanikisha Safari ya Mama huyo kutoka Hospitali ya Wazazi Meta hadi
kijijini kwao umbali wa Kilomita zaidi ya 130, Mwenyekiti wa Kijiji cha
Chiwanda, Ignas Sinkara aliwapongeza waandishi hao kwa moyo walioonesha na
kuwaomba kuendelea kujitolea hivyo hivyo katika majukumu mengine.
Alisema moja ya michango iliyopatikana
imesaidia huduma za mama alipokuwa Hospitali, kukarabati Nyumba atakayoishi
baada ya kujifungua pamoja na kusaidia shughuli za Shamba kutokana na wazazi
wote wawili kutakiwa kusaidiana katika kuwahudumia watoto hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji
cha Mpumpi anapotokea Mama huyo, Winstoni Mtali, alisema mbali na juhudi
zilizopangwa na serikali ya kijiji pamoja na wasamaria wema walionesha kuguswa
na mama huyo tangu alipojifungua bado misaada zaidi inahitajika kutokana na
mzigo huo kuwa mkubwa kwa Wanakijiji.
Alisema bado mazingira ya nyumbani kwa
mwanamke huyo na kijiji kwa ujumla siyo rafiki kwa malezi ya watoto hao
kutokana na nyumba yao kutokuwa katika mazingira mazuri hivyo kuhitajika
michango ya hali na mali kwa ajili ya ukarabati wa nyumba hiyo ambayo inahitaji
kusakafiwa, kupigwa dali, madirisha na kusakafia kuta ili watoto wasidhurike na
vumbi la ndani
Waandishi waliojitolea kufanikisha
safari ya Mwanamke huyo hadi kijijini kwao ni pamoja na Venance
Matinya(JamboLeo), Ezekiel Kamanga(Bomba Fm Redio), Joseph Mwaisango ambaye ni
mmoja wa wakurugenzi wa mtandao wa
kijamii wa Mbeya yetu Blog na Jacob Mwaisango aliyejitolea gari lake.
Namba ya mama wanne yaani mapacha wanne ni
0769 12 51 88
au
mwenyekiti wa kijiji
0783 87 59 99
Na Mbeya yetu
|
4 comments:
KAZI NZURI
NAWAPONGEZA SANA MBEYA YETU KWA MLICHOMFANYIA HUYU MAMA MUNGU ATAWABARIKI
Mpaka namaliza kuisoma hii habari machozi ya furaha yamenitoka.
Mungu ambariki mama wanne pamoja na wote mliofanikisha mpaka pale alikofikia.
Naahidi kusafiri kuja Mbeya kumuona mama wanne.
Baba wanne.....hongera, sasa naamini utawekeza zaidi kwenye elimu za wanao.
Naahidi kuja kuwatembelea.
JAMBO JEMA SANA
Post a Comment