WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa
wingi kujiunga katika Mifuko ya kijamii hususani Mfuko wa Pensheni wa
PSPF Kutokana na maboresho na huduma zake zinazolenga kuwanufaisha wananchi wa
ngazi zote.
Mwito huo umetolewa na Afisa Uendeshaji
wa PSPF Makao makuu Dar Es Salaam, Murua Kihore katika mahojiano maalumu na
mwandishi wa habari hizi katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea
katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya.
Kihore amesema lengo la PSPF kuwepo
katika maonesho hayo ni kutoa Elimu kwa Wananchi wote bila kujali itikadi,
utaifa wala dini kuhusu mafao mapya yalioanzishwa na mfuko huo ambayo yamelenga
watu wa ngazi zote kama watumishi wa umma, wafanyabiashara na wajasiliamali
wenye uwezo wa kuchangia mfuko kwa hiari.
Amesema mafao mapya yalioanzishwa kwa
watu wote ni pamoja na mafao ya elimu, Ujasiliamali, mafao ya uzeeni, mafao ya
kifo, mafao ya kujitoa, mafao ya ugonjwa na mafao ya ulemavu.
Ameongeza kuwa kutokana na sheria na
sheria mpya ya mifuko ya kijamii inayotaka kila mwananchi kupata fursa sawa
katika hifadhi za kijamii, ndiyo maana PSPF imejikita katika kutoa elimu kwa
wananchi kujiunga na mfuko huo kutokana na faida watakazo zipata baada ya kuwa
wanachama.
Amesema hivi sasa PSPF iko kwenye
mkakati wa kubadilisha majina yake kutoka kuwa mfuko wa pensheni kwa watumishi
wa umma na kuwa mfuko kwa kila mtu kutokana na baadhi ya watu kuamini kuwa
mfuko huo upo kwa ajili ya watumishi wa umma tu.
Kwa upande wake Amina Mtingwa, Afisa
Mwendeshaji wa mfuko wa PSPF kutoka Makao makuu amesema mfuko huo unafaida
kubwa kwa wajasiliamali wenye vipato vya kawaida kwa sababu zimefunguliwa ofisi
Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani ambapo pia mwanachama anaweza kupata
taarifa za mfuko popote atakapokuwepo kupitia mitandao pamoja na mafao kufika
kwa wakati mteja anapohitaji.
Amezitaja baadhi ya kazi za mfuko kuwa
ni pamoja na kusajili wanachama wapya kwenye mfuko, kukusanya michango kutoka
kwa wanachama, kufanya uwekezaji katika vitega uchumi vilivyosalama na kulipa
mafao kwa wanachama aliyekamilisha taratibu.
Afisa huyo amezitaja baadhi ya njia
ambazo mchangiaji anaweza kuchangia mfuko huo kuwa ni pamoja na Tawi la Benki
ya NMB Kupitia akaunti namba 20101100085 kwa jina la Public Service Pension, au
CRDB kwa jina hilo hilo namba 01J1120380700 na kupitia mitandao ya simu ya
Mpesa na Tigo Pesa.
Ameongeza kuwa Mchangiaji huyo anaweza
kuchanga kadiri anavyopata ambapo kima cha chini ni Shilingi 10,000 kwa Mwezi
ambazo Mtu yoyote anaweza kutoa fedha hizo aidha kwa wiki, mwezi, msimu au kwa
Mwaka ili mradi azingatie kima cha chini cha uchangiaji.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment