Meneja masoko wa kampuni ya uzalishaji wa Mbegu ya Highlands Seeds, John Mbele, wa pili kushoto akionge na mwandishi wetu
WAKATI watanzania wengi wakielekea
katika msimu wa kilimo, wameshauriwa kuwa makini na wauzaji wa pembejeo za
kilimo ili kuepuka kuuziwa mbegu zisizokuwa na ubora na kuingizwa kwenye
umaskini.
Rai hiyo imetolewa na Meneja masoko wa
kampuni ya uzalishaji wa Mbegu ya Highlands Seeds, John Mbele, katika maonesho
ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa
Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya.
Amesema baadhi ya wafanyabiashara siyo
waaminifu na kuwauzia wakulima mbegu feki ambazo wakizipanda hazioti au zikiota
hushindwa kutoa mazao yenye tija kwa mkulima.
Amesema ili kukabiliana na adha hiyo ni
vema wakulima wakawa wanadai risiti baada ya kununua mbegu kutoka kwa muuzaji
au wakala ili pindi zinapomletea madhara ili rahisi kumchukulia hatua za
kisheria.
Akizungumzia Mbegu wanazoshughulika nazo
za Mtama, Alizeti, Ufuta, Mtama na mahindi kuwa ni mkombozi kwa mkulima
kutokana na kufanyiwa utafiti na kuzalishwa hapahapa nchini kwa kuzingatia
mahitaji ya Watanzania.
Amesema mbegu za kutoka Highlands Seeds
zinastahimili magonjwa, ukame pamoja na kutokuwa na pumba nyingi kuliko unga
jambo ambalo ni mkombozi kwa mkulima na mwanachi wa kawaida kwa sababu ya
kumwingizia kipato.
Meneja huyo ameongeza kuwa wapo matapeli
wengi wanaotumia majina na nembo za kampuni hiyo kuzalisha mbegu zisizokuwa na
ubora kwa lengo la kuharibu biashara na kuwarudisha nyuma wananchi kimaendeleo
na mapato kwa ujumla.
Amesema ili kuepuka adha hiyo wakulima
wameshauriwa wanaponunua mbegu kuhakikisha wanadai risiti na kutotupa mifuko
waliyonunulia ili iwe rahisi kuwabana wauzaji matapeli.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment