Pf3 ya polisi
Wiki ya
kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto ikiwa imeanza kuadhimishwa
duniani Novemba 25 mwaka huu bado vitendo hivyo vimezidi kushamiri Mkoani Mbeya
ambapo mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Aiport Kata ya Iyela jijini Jacline
Staniely[9] kuumizwa mkono wake wa kushoto.
Jacline
akiongea kwa ridhaa ya mama yake amesema alipigwa kwa kutumia ubao na mwalimu
wa shule hiyo Novemba 19 mwaka huu na mwalimu Kanyika kwa kosa la kuwa na
nywele ndefu.
Mwanafunzi
huyo amedai kuwa siku ya tukio alipigwa vibaya na kumsababishia maumivu makali
ambapo siku hiyo mama yake alikuwa safarini Nairobi Kenya hivyo hakupata
matibabu ambapo alilazimika kumwambia mwalimu jirani[Bibi]ambaye alimpeleka
hospitali kutibiwa.
Hata hivyo
Jackline amesema kuwa kutokana na maumivu makali alilazimika kufanya mtihani wa
Taifa wa darasa la nne bila kupata matibabu ya kutosha.
Baada ya
kurejea kutoka safari mama yake mzazi aitwae Rehema Adamson Ndeje[28] mkazi wa
Block T jijini Mbeya amesema baada ya maumivu ya mwanae usiku ilimlazimu kwenda
shuleni ili kujua kulikoni,ndipo alipoonana na mwalimu Kanyika baada ya
kukutanishwa na Mwalimu mkuu.
Mama Jackine
amesema hicho ni kipigo cha tatu kukubwa kwa mwanae kupigwa na mwalimu huyo
ambapo alionesha makovu yaliyodaiwa yalitokana na vipigo vya mwalimu huyo
miguuni akidai majeraha hayo yalidumu kwa miezi mitatu.
Hata hivyo
Rehema aliamua kwenda Polisi Mwanjelwa kutoa taarifa za tukio na kila alipoitwa
mwalimu huyo hakutokea ndipo jalada likapelekwa kituo kikuu cha kati ambapo
mwalimu alikamatwa na mhanga kupewa PF 3 kwa ajili ya matibabu ambapo alipigwa
picha na kuonekana moja ya kidole cha kati cha kushoto kuoneka kuathirika
kutokana na kupigwa kwa kutumia ubao.
Mzazi huyo
amesema hana ni mbaya na mwalimu Kanyika lakini kitendo cha kumwadhibu mwanae
mara kwa mara ndicho kimemtia shaka hata kuamua kutoa taarifa Polisi ili sheria
ichukue mkondo wake.
Mwandishi wa
habari hii alipofika shuleni ili kujua mustakabali wa suala hili mwalimu alitoa
nje mwandishi akidai yeye ana majukumu mengine lakini baada ya kufuatilia mkuu
huyo alichukua gari lake aina ya RAV 4 na kwenda nyumbani kwa Mzazi wa mtoto na
kwenda naye hospitali akiwa ameambatana na mmoja wa walimu wa shule hiyo ambaye
ni jirani ambapo Jackline humwita Bibi.
Mwandishi
alimtafuta mmoja wa wanaharakati wa kijinsia ambaye alikiri kupokea lalamiko
hilo ingawa alijibu kwa mkato kuwa mtoto huyo kaumia kidogo tu na ni usanii
mtoto huyo kufungwa POP na kwamba bado PF3 haijajazwa kitu hivyo hawezi
kuzungumzia lolote.
Kumekuwa na
malamiko mengi katika Dawati hilo kutokana na matukio kutochunguzwa kwa wakati
hali inayotoa mwanya kwa vitendo hivyo kuibuka mara kwa mara na wahalifu
kutoroka mkono wa sheria lakini baadhi kuwa na utendaji duni licha ya taarifa
kutolewa kwa wakati.
Kamanda wa
Polisi Mkoani Mbeya ameahidi kulifuatilia suala hilo na ikibainika mtuhumiwea
atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
1 comment:
Hakika huu ni ukatili usio kifani...ni mwalimu mwananke au? Pole Jacline kwa maumivu. Natumaini mambo kama haya yatakuwa yanafuatiliwa kikamilifu
Post a Comment