Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, November 27, 2013

TRA MBEYA YASEMA WAFANYABIASHARA WAKUBWA WANAWATUMIA MACHINGA KUANDAMANA.

Add caption


MENEJA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mbeya, Arnold Maimu amesema wanaogomea kutumia mashine za Kielotronik(EFD) ni wafanyabiashara wadogo ambao hata mashine hizo haziwahusu.
 
Aliyasema hayo jana wakati akijibu swali kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe alipotembelea banda ya maonesho la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya kibiashara yanayofanyika katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya.
 
Maimu alisema wafanyabiashara wanaopaswa kutumia mashine hizo ni wake tu wenye uwezo wa kuingiza Milion 14 pamoja na wafanyabiashara wote wenye viwanda, biashara za jumla na rejareja, waliosajiliwa na ongezeko la thamani(VAT) na wale wote ambao wataamuliwa na Kamishina wa TRA kutumia mashine hizo.
 
Alisema mara nyingi wanaoonekana barabarani na kupinga matumizi ya mashine hizo ni wafanyabiashara ambao hawahusiki na wala hawajatajwa bali wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa.
Mwisho.

Na Mbeya yetu
 

No comments: