Polisi wakiondoka na mwili wa marehemu
MTU
mmoja asiyefahamika jina wala makazi yake, amepoteza maisha baada ya kupigwa na
kuchomwa moto na wananchi ambao wameamua kujichukulia sheria mkononi.
Wananchi
hao ambao ni wakazi wa eneo la Mtakuja Mbalizi, walifanya tukio hilo jana
majira ya saa mbili asubuhi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtakuja Mbalizi Mbeya vijijini, Ambonisye
Masinga, alisema kuwa marehemu huyo alidaiwa kuiba pikipiki eneo la
Utengule.
Alisema,
baadhi ya madereva wa bodaboda(pikipiki) walianzisha msako na kufanikiwa kumtia
nguvuni marehemu huyo na kuanza kumshushia kipigo huku mwili wake ukiwa
umefungwa kwenye pikipiki na kuuburuza barabarani umbali wa kilomita moja.
Alisema,
mwili huo uliburuzwa na kufikishwa kwenye eneo la mlima reli maarufu kwa jina
la eneo la adhabu kwa wahalifu na kuchoma moto mwili wake.
Aidha,
katika tukio hilo fundi ujenzi aliyekuwa katika eneo hilo Asangalwisye
Mayasu(50) mkazi wa kivukoni, alijikuta akiambulia kipigo baada ya kujaribu
kuwazuia wananchi ambao waliamua kujichukulia sheria mkononi.
“Baada
ya msamalia huyu kupigwa na kuumizwa vibaya serikali ya kijiji ilimkimbiza
hospitali Teule ya ifisi na kwamba hali ya afya yake si nzuri hali iliyopelekea
mke wake aitwaye Kristina Kyando (45) Kuzirai,”alisema
Hata
hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi litahakikisha linawatia mbaroni watu
wote waliohusika na mauaji hayo.
Kumeibuka
kwa vitendo vya madereva pikipiki kujichukulia sheria mkononi ambapo hivi
karibuni walifunga barabara ya Iwambi Jijini Mbeya kwa kulishinikiza jeshi la
polisi kuwaachia watuhumiwa wawili ambao walituhumiwa kuiba pikipiki ili
wawaue.
Mwisho.
Picha na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment