Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, October 25, 2013

Uongozi wa timu ya Mbeya city Fc inayoshiriki ligi kuu ya vodacom Tanzania bara unakujulisha kuwa mechi kati ya mbeya city na Tanzania prisons iliyokuwa ichezwe jumamosi ya tarehe 26/10/2013 imeahirishwa hadi tararehe 29/10/2013.





Uongozi wa timu ya Mbeya city Fc inayoshiriki ligi kuu ya vodacom Tanzania bara unakujulisha kuwa mechi kati ya mbeya city na Tanzania prisons iliyokuwa ichezwe jumamosi ya tarehe 26/10/2013 imeahirishwa  hadi  tararehe 29/10/2013.

sababu ni Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufanya marekebisho ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ili kupisha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania na Msumbiji.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza kwa mashindano ya wanawake wenye umri chini ya miaka 20 itachezwa Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.

Hivyo basi vituo vitakavyotumika kuuza tiketi katika mechi hiyo ya mbeya city na Tanzania Prisons ni vifuatavyo Ilomba, Kabwe, Mwanjelwa, Sokoine uwanjani, Stendi  ya mabasi yaendayo mikoani, pamoja na Uyole.

kiingilio katika mechi hiyo ni shilingi elfu tano tu.

Pia uongozi unawaomba mashabiki na wananchi kwa ujumla wetu kudumisha amani na utulivu katika mechi hiyo.


Freddy Jackson, Afisa habari Mbeya City Fc


1 comment:

Clara said...

Inapendeza sana kuona timu mbalimbali zinashiriki mashindano mkoani Mbeya. Ombi langu ni uwanja wa Jiji la Mbeya hauna hadhi kama jiji jamani, ikiwezekana ukusanyaji wa pesa ufanywe ili uwanja ujengwe kwa hadhi ya kimataifa. Asanteni