Uongozi wa timu ya Mbeya city Fc inayoshiriki ligi kuu ya vodacom
Tanzania bara unakujulisha kuwa mechi kati ya mbeya city na Tanzania prisons
iliyokuwa ichezwe jumamosi ya tarehe 26/10/2013 imeahirishwa hadi
tararehe 29/10/2013.
sababu
ni Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufanya
marekebisho ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ili kupisha mechi ya mchujo
ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania na Msumbiji.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza kwa mashindano ya wanawake wenye umri chini
ya miaka 20 itachezwa Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 10 jioni.
Hivyo
basi vituo vitakavyotumika kuuza tiketi katika mechi hiyo ya mbeya city na
Tanzania Prisons ni vifuatavyo Ilomba, Kabwe, Mwanjelwa, Sokoine uwanjani,
Stendi ya mabasi yaendayo mikoani, pamoja na Uyole.
kiingilio
katika mechi hiyo ni shilingi elfu tano tu.
Pia
uongozi unawaomba mashabiki na wananchi kwa ujumla wetu kudumisha amani na
utulivu katika mechi hiyo.
Freddy
Jackson, Afisa habari Mbeya City Fc
|
1 comment:
Inapendeza sana kuona timu mbalimbali zinashiriki mashindano mkoani Mbeya. Ombi langu ni uwanja wa Jiji la Mbeya hauna hadhi kama jiji jamani, ikiwezekana ukusanyaji wa pesa ufanywe ili uwanja ujengwe kwa hadhi ya kimataifa. Asanteni
Post a Comment