MAMA huyo aliyejulikana kwa jina la
Mariamu Mponzi anakadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 80 na 85 ambaye ndiye
mama mzazi na Emmanuel Yuta muuzaji wa nyumba hiyo ametoa ya moyoni baada ya
kufanikiwa kuigomboa nyumba kutoka kwa mnunuaji.
Kikongwe hiyo alichukua hatua hiyo baada
ya kubaini kuwa kitendo kilichofanywa na mwanae akishirikiana na serikali ya
kijiji si cha kiungwana cha kuuza nyumba ya familia na kuwaacha watoto wasijue
la kufanya.
Aidha alilazimika kukopa fedha toka kwa
majirani jumla ya shilingi 410,000/= ambazo mnunuzi Dati Nsagaje alidai
arudishiwe ili naye aachie nyumba hiyo jambo ambalo bibi huyo alifanikiwa, hata
hivyo nyumba mbili pamoja na uwanja viliuzwa kwa jumla ya shilingi 750,000 na
mnunuaji alitoa kianzio cha shilingi 400,000/= na shilingi 10,000/= alidai ni
usumbufu alioupata.
Akizungumza baada ya kurejesha nyumba
hiyo kikongwe huyo alisema kwa sasa nyumba hiyo ni mali ya wajukuu zake hivyo
mwanae akishindwa kuendelea na maisha alikokimbilia na kuamua kurejea nyumbani
asikanyage katika nyumba hizo bali akatafute mahali pengine pa kuishi.
Alisema inaweza ikamfikia taarifa kuwa
nyumba imerudishwa hivyo hapa hatatakiwa kukanyaga kwa sababu hiyo ni mali ya
wajukuu zake na yeye itambidi kutafuta eneo lingine na kuanza upya kujenga.
Mkasa huo wa ajabu ulitokea katika kijiji
cha Hatwelo, Kata ya Ijombe Mbeya Vijijini ambapo Mkazi huyo aliyefahamika kwa
jina la Emmanuel Yuta alipouza nyumba yake na kutokomea yeye na mkewe na
kuwaacha watoto wawili wenye umri kati ya miaka 9 na 11 wakikosa mahala pa
kuishi.
Kutokana na kitendo hicho kutokubalika,
baadhi ya Majirani walisema ni
kitendo cha kinyama na hakipaswi kufumbiwa macho ambapo waliamkopesha fedha ili
kuikomboa nyumba ili irudi mikononi mwa watoto.
Baada ya kupata fedha hizo, Kikongwe huyo
alitoa shilingi 410,000/= alizokuwa amedai mnunuaji ili aweze kurejesha nyumba
ikiwa ni fedha alizokuwa ametoa awali hivyo kukubaliana kuicha nyumba hiyo
ambayo kwa mujibu wa majirani na baadhi ya ndugu wamesema itakuwa ni mali ya
watoto.
Alisema hadi sasa amefanikiwa kurudisha
fedha kiasi kwa waliomkopesha na bado anadaiwa shilingi 100,000/= anazotegemea
kurudisha baada ya kuuza viazi anavyolima yeye mwenyewe kutokana na hali ya
mumewe kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya magonjwa na uzee.
Aidha juhudi za bibi huyo kuikomboa
nyumba hiyo na kuwa mali ya watoto zilifanikiwa ambapo mnunuzi Datistani
Mwanshinga alibatilisha ununuzi wa nyumba hiyo Mei 9, Mwaka huu baada ya kukiri
kurejeshewa fedha zake.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment