Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, October 22, 2013

HOT NEWS: SUGU NA MWANJELWA WADAIWA KUGOMBANISHWA



*Nia ni kubadili ajenda ya maendeleo ili yawe malumbano

Na Gordon Kalulunga, Mbeya

KAULI iliyoandikwa hivi karibuni kuwa Waziri wa Maendeleo Jinsia na watoto, Sophia Simba kwamba Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ana mapepo, imeelezwa kuwa imelenga kubadili ajenda ya maendeleo katika Jiji la Mbeya na kuwaingiza katika malumbano Mbunge huyo na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa.

Hayo yameelezwa na wananchi na baadhi ya wanasiasa waliokuwepo eneo la mkutano na kwamba kauli hiyo haikutolewa na viongozi hao bali ilitolewa na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa Taifa kupitia wilaya ya Mbeya mjini, Charles Mwakipesile.

Mwakipesile, ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, katika mkutano wa Sophia Simba, alisema Mbunge Joseph Mbilinyi(Sugu), alipagawa na pepo wachafu ndiyo maana aliingilia ugomvi ambao haukumhusu na kuamua kupigana wakati muhusika(Freeman Mbowe) hakukataa kutoka nje.

‘’Kwasababu yeye hana hoja na alikuwa amekosa cha kuzunguza kuhusu mswada wa katiba, hivyo aliona ili aonekane kwenye luninga ni vema akaingilia suala ambalo halikumhusu maana katika jimbo lake ameshindwa kutekeleza ahadi ya kujenga mabwawa ya samaki katika kata 36 za Jiji la Mbeya kama alivyowaahidi wananchi’’ alisema Mwakipesile.

Walisema kuwa inashangaza kuona baadhi ya waandishi wa habari kuamua kwa makusudi kutumika na kuhamisha maneno ya Mwakipesile na kumlisha Dr. Mwanjelwa ambaye hakugusia wala kuunga mkono kauli hiyo iliyoelekezwa kwa Mbunge Sugu.

Akihojiwa na Mtandao huu wa www.kalulunga.blogspot.com Dr. Mary Mwanjelwa alisema kuwa amechafuliwa lakini ni vema jamii ikaelewa kuwa sera yake yeye siyo kulumbana bali ni kufanya kazi na kutekeleza ilani y chama chake (CCM).

‘’Walioandika kitu ambacho sikukisema mimi hawajanitendea haki, wanataka kunigombanisha bure na mbunge mwenzangu na huu ni uchochezi, lakini siwezi kurudi nyuma kuwatumikia kimaendeleo wananchi wa Jiji la Mbeya na mkoa kwa ujumla’’ alisema Mwanjelwa.

Hayo yamekuja baada ya siku mbili baada ya Waziri Sophia Simba ana Mbunge huyo kudaiwa kumkejeli Sugu, kuwa awapo bungeni anaongozwa na mapepo wakati Sugu anasema anayoyafanya yote yana Baraka kutoka kwa wananchi wa jimbo lake la Mbeya Mjini.


No comments: