Agustino Steven (8) akiandaa ugali ale na dada yake |
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakichambua mboga aina ya mchicha |
Agustino Steven (8) akipika mchicha |
Hii ndiyo sahani yao wanayotumia kwa ajili ya chakula |
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) hapa wakila chakula walichopika wenyewe |
Unga pamoja na maharage |
Hili ndilo sanduku lao |
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakiwa nje ya nyumba wanayoishi
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili
wenye umri wa miaka saba na nane wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi
matano bila huduma za msingi.
Watoto hao wamefahamika kwa majina ya
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la
kwanza shule ya msingi Mapambano
iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto
hao wamesema Wazazi wao waliwaacha kwenye nyumba ya kupanga tangu mwezi wa Mei
mwaka huu ambapo Baba inasadikika alielekea Umalila Mbeya Vijijini ambako
inasemekana ameoa mke mwingine.
Wamesema Mama yao alielekea Mbozi ambako
pia naye inasadikika ameolewa na mwanaume mwingine hivyo kuwaacha watoto bila
kuwa na huduma za msingi kama Chakula na mavazi huku wakiwa wameachiwa Nyumba mtaa wa Jakaranda Airport.
Aidha watoto hao waligundulika baada ya
kukutwa mitaani wakitafuta riziki kwa kuzoa taka kwenye majumba ya watu kisha
kupeleka majalalani kwa ujira wa kati ya shilingi 200 na 500 ambazo huzitumia kununua mahitaji ya
nyumbani pamoja na kujipikia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la
Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio
na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia
jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za
kisheria.
Amesema majirani pia waendelee kuwa
karibu na watoto hao hadi pale wazazi wao watakapopatikana kwa kuwahudumia na
kuhakikisha wanaendelea na masomo kama kawaida.
Amesema kitendo kilichofanywa na wazazi
hao ni cha kinyama hivyo wakipatikana hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ambapo
pia alitoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya kikatili.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mtandao
huu wa www.mbeyayetu.blogspot.comumebaini kuwa Wazazi hao wanatabia kama hiyo kutokana na kuwahi kumtelekeza
binti yao mwenye umri wa miaka 17 aliyefahamika kwa jina la Salome Steven
ambaye hakuwahi kupelekwa shule hivyo kuachiwa jukumu la kuwalea wadogo zake.
Kutokana na ugumu wa maisha binti huyo
katika harakati za kutafuta chochote kwa ajili ya wadogo zake ameishia
kuzalishwa mtoto wa kiume ambaye ana mwezi mmoja sasa na kuwakimbia wadogo zake
nay eye kukimbilia kwa rafiki yake.
Pia Jeshi la Polisi kupitia dawati la
Jinsia limeamua kulifuatilia suala hilo kwa kumtafuta kijana aliyemzalisha
binti huyo aliyefahamika kwa jina moja la Hezron ambaye imedaiwa kuwa walikuwa
wakikutana kwenye nyumba ya kulala wageni(Gesti ).
Na mbeya yetu
****** KAMATA FURSA YA BIASHARA SASA! Je unapenda kuwa Mjasiriamali na kutengeneza kipato endelevu huku ukiwa unajifunza Ujasiriamali? Je unamalengo makubwa , unapenda kujituma na kujifunza na umri wako ni kuanzia Miaka 18? Kama Jibu ni Ndio Basi Piga simu hii au Tuma ujumbe mfupi wa maneno na utapigiwa simu Fasta.. Namba ni +255716742234. Wahi sasa!! |
4 comments:
Inasikitisha inaumiza, kwa kweli kuna wazazi wengine wana roho ya ukatili,hivi siku hawa watoto wakikua na wakiwa na kazi zao, wazazi wao watajivunia kuwa ni watoto wao?
Ndugu mwandishi mimi binafsi nimeguswa sana na hao watoto kuishi mazingira. Ila ingekua vizuri kama ungeweka wazi uwezekano wa hao watoto kusaidiwa kwa namna yoyote.au kama kuna anawaangalia kwa sasa atoe mawasiliano mtu mwenye chochote tuweze kutuma msaada wowote tulionao. Pia ungeomba waandishi wenzako blogu kubwa kama mimi Michuzi, kule ni rahisi kusaidiwa hao watoto. Inasikitisha sana.
Hao watoto wanaangaliwa na nani mpaka sasa, wakati jamii ikitafuta wazazi wao? Au ndio huruma za mamba?
Serikali inapaswa kuchukuwa hatua kali sana kwa wazazi wa namna hii...
Jambo lingine ni vema kuwa na vituo maalum vya kulelea watoto ambao wametelekezwa na wazazi wao ili kukinusuru kizazi hiki ambao ndio vijana wa kesho... Hawa watoto na wengine kama hawa kama hawata angaliwa vema, ndio watakao kuwa aidha majambazi wa kesho au wenye kufanya biashara ya kujiuza... Kuna haja ya jamii kuamka na kuliona ili, maana tunatengeneza jinamizi ambalo litakuja kutumaliza kesho na kesho kutwa...!
munguawajalie majiran roho ya huruma na upendo ili kuwajali watoto hao
Post a Comment