Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, October 23, 2013

CHARLES MWAKIPESILE, AKANUSHA KUHUSU KAULI ZA MAPEPO NA KUELEZA KILICHOJILI MKUTANO WA CCM KATA YA MAANGA

 MJUMBE wa mkutano mkuu wa taifa(CCM) Charles Mwakipesile kupitia wilaya ya Mbeya mjini,





Kwa siku  tatu sasa  kumekuwa na malumbano kwenye vyombo vya habari
kuhusiana  kauli zilizotamkwa na viongozi  watatu  wakiongozwa na
waziri wa maendeleo ya jamii jinsia  na watoto  Bi.Sophia  Simba
,mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya  (CCM) Dkt.Mary Mwanjelwa
wakati wa mkutano wa  hadhara  katika  kata  ya  Maanga .

Mkutano  huo uliokuwa unasimamiwa na katibu wa wilaya wa CCM
Mwl.Raymond Mwangwala  ulikuwa na mkubwa  uliokuwa na shamra  shamra
kubwa  zilizotokana na  wananchi wengi kuitikiwa na kufurahia
burudani na jumbe mbali mbali zilizokuwa zinatolewa.
Katika  mkutano huo  viongozi wengi walipata nafasi ya kutoa  salamu
wakiwemo  viongozi  hao ambao wamekuwa wakitajwa  katika  vyombo vya
habari (magazeti)  ambao ni waziri Simba  na Mbunge  Dkt.Mwanjelwa
wakionekana  wazi  kuwa walimshambulia  Mbunge  Sugu kuwa ana  mapepo
jambo  ambalo kwa hakika si  la  kweli  kabisa “ baadaye  habari hizo
zimekanushwa na katika  moja  ya Blog  moja  Mkoani Mbeya  zikidai
kuwa  aliyemtaja mbunge  huyo ni  Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa
Charles Mwakipesile .

Kwa  ajili ya maslahi  ya watanzania  na wafuatiliaji wa mambo ya
kisiasa  ukweli  ni kuwa  mbunge  Joseph Mbilinyi  hakushambuliwa
katika mkutano huo wala kutajwa  jina  lake  badara  yake  viongozi
hao wa  CCM walichofanya  ni kueleza  mambo ya maendeleo yaliyofanywa
na  chama hicho  kwa ajili ya kujenga  hoja  kwa wananchi  wengi
waliokuwa wanasikiliza .

Akitoa salamu  mjumbe wa Mkutano  mkuu  Taifa  CCM Bw.Mwakipesile
ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari alisema kuwa  yeye  kama mzee
wa kukemea  mapepo  siku  zote anacho amini ni kuwa  wenye mapepo kazi
yao ni kufanya  fujo  wakati  viongozi wa CCM wanajenga  hoja
,”wakati wao wanafanya fujo bungeni  CCM tunajenga  hoja,wakati wao
wanachoma  barabara sisi tunajenga  barabara kila kona ,wakija kwenu
waulizeni samaki walizo ahidi ziko wapi wajenge  hoja  waacha kutukana
,

akamalizia kwa kuwataka  wana Mbeya kuendelea  kuwa na mshikamano
amani na utulivu  na kumwakikishia  waziri  Simba  kuwa pamoja na
kuwapo  kwa  mapepo kidogo  Jiji liko safi”tupelekee salamu kwa
mwenyekiti wa CCM  Taifa  Dkt.Jakaya Kikwete  kuwa Mbeya  iko safi
CCM inachapa  kazi.Mwisho wa salamu.

Mbunge wa Viti maalumu  Mkoa wa Mbeya  Dkt.Mwanjelwa  ambaye pia ni
mjumbe wa Halmashauri kuu CCM kupitia  UWT,akitoa  salamu alijikita
katika kueleza  mambo  ya maendeleo  ambayo wakati wote amekuwa
akifanya    awapo  Mbeya  na Bungeni Dodoma  ambapo alisema kuwa mradi
mkubwa ambao amekuwa akiusimamia baada ya kuuliza  swali  ni ule  wa
kuchepusha  barabara kutoka  uyole  kuibukia  Songwe kwa lengo  la
kuondoa  msongamano wa magari  Jijini Mbeya barabara kuu iendayo
Zambia .

Huku akishangiliwa mbunge huyo alisema kuwa  mbali na  mpango huo pia
amekuwa akizukuma  maendeleo ya  Mkoa  wa Mbeya  kwa ajili ya
kuhakikisha makundi  mbali mbali  wakiwemo wanawake  wanapata maisha
bora ikiwa ni kutimiza  sera  ya  CCM katika  suala  zima  la
kusimamia  utekelezaji wa ilani”akamaliza  kwa kusema  mambo
aliyofanya ni mengi  ila kwa kuwa muda  hautoshi  kwa siku hiyo  hayo
machache  yanatosha.

Naye  mgeni  rasmi katika  mkutano huo  Bi.Simba ambaye  kitaaluma ni
mwanasheria  akihutubia  wananchi hao alionya tabia ya  wazazi
kuwanyanyasa  watoto  kwa kupuuza haki zao za msingi  jambo ambalo
alilaani vikali  na kuwa serikali kamwe haifumbia mambo  jambo hilo.

Pia alizungumzia  jinsi ambavyo serikali  ya CCM inafanya kazi kubwa
katika  kuhakikisha  wanawake na  vijana  wananufaika kwa mikopo
kutokana na asilimia 10 ya mapato ya  ndani ya Halmashauri ambayo
inatakiwa kila mwaka itolewa  kwa ajili ya kuwawezesha kupata maisha
bora.

“serikali  ya CCM ni sikivu na makini  ndio maana  mnaaona hata  pale
bunge  sisi tulifanya kazi kubwa ya kujenga  hoja  kwa utulivu lakini
wenzetu  siku  ni kwa sababu  ya  mapepo  wao wakaamua kupigana  bila
ya sababu jamani  ilikuwa ni aibu  kama mnavyofahamu pale  bungeni  ni
mahari  patakatifu  hivyo hata  watu wanaoingia  pale  wanapaswa kuwa
makini  tena siku  ile  yalilipolipuka mapepo  wachungaji  akina
Dkt.Lwakatare  hawakuwepo  wangekemea  ,lakini  nasikitika  Mbeya
nanyi mlituletea  pepo mnaona kilichofanyika .

Waziri  Simba  alitoa  hotuba  yake  mwanzo mwisho bila  kumtaja  mtu
kwa jina  wala kumshambulia ,Dkt.Mwanjelwa  alitoa  salamu zake bila
kumtaja mtu  wala kumshambulia  na kisha  mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa
CCM  Mwakipesile alitoa  salamu kwa  kutumia  kauli mbiu yake  yam
zee wa kukemea  mapepo bila  ya kumshambulia wala kumtaja  mtu.
Mfumo wa  vyama  vingi uulikubaliwa nchini kwa ajili ya kuchochea
maendeleo na kutoa  changamoto kwa chama tawala , wala si ugomvi
unaopelekea  viongozi  wakiwemo wabunge  kushindwa  kuelewana  kwa
kisingizio cha  utofauti wa itikadi, hii  kwa  hakika  si lengo la
kuwapo kwa mfumo huu wa vyama  vingi ambao unalenga  kuheshimiana  na
kuacha kudhalilishana ,WAJIBU WA KULINDA  NA KUSIMAMIA  MSHIKAMANO HUU
WA VIONGOZI UKO MIKONONI  KWA SEHEMU KUBWA KWA WANA HABARI ambao
wanasisitizwa na  sheria  kufanya kazi ya kuwaunganisha viongozi na si
kuwagonganisha (TO LINK LEADERSHIP TO THE PUBLIC) and also to Bind A
society  kwa  msingi huu makosa  yaliyojitokeza  katika  habari hii
yaliyolenga kuwasambaratisha  wabunge  kwa kisingizio cha  uchaguzi
2015 hayana  msingi kwa sasa  wana  Mbeya  wanachohitaji ni maendeleo
kutoka  kwa viongozi  hao  kuwasemea  kuwa  wana ugomvi hiyo siyo
kweli  kwa kuwa:

Ukweli ni kuwa  kila mmoja  miongoni mwao anafanya kazi kwa ajili ya
kuwahudumia wana nchi akitekeleza  ilani ya chama  chake  na hivyo
ukweli  ni kuwa  katika  Mkutano huo  Viongozi  hao wakuu wawili kwa
maana  ya Waziri Simba  na mbunge  Mary Mwanjelwa  hakuna  walipomtaja
  Mbunge  Mbilinyi kuwa ana Mapepo  na wala  Mjumbe  wa Mkutano mkuu
Taifa  CCM  Bw.Mwakipesile  hakuna alipomtaka  Mbunge  huyo  ana
Mapepo kilichoandikwa ni upotoshwaji  mkubwa  usio na lengo bora na
siasa  za Mkoa  wetu wa Mbeya .
Mwananchi     Halisi.

3 comments:

Anonymous said...

WAO WANAOKUMBATIA MAFISAD NDO MAPEPO

Anonymous said...

WAO WANAOKUMBATIA MAFISAD NDO MAPEPO

Anonymous said...

Kumbe hakutajwa mtu?! Lkn Mh Simba kasema Mby walipeleka pepo, alimaanisha nn? Bila shaka hicho ndicho kilichotafsiriwa kumtaja Sugu. Nadhani chanzo cha tatizo ni aliyetoa hoja na si waliotafsiri.