Wananchi waHALMASHAURI YA BUSOKELO Wilaya ya RUNGWE Mkoani
MBEYA wajadili rasimu ya Katiba katika mchakato unaoendelea nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyokuwa ya kiraia
inayojumuisha waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya inayojulikana kama ELIMISHA,
FESTO SIKAGONAMO amesema lengo ya asasi hiyo ni kuwapa fursa wananchi wa
vijijini kuweza kutoa maoni yao katika mchakato wa Katiba
Baadhi ya wananchi wamependekeza serikali moja ya Muungano
ili kupunguza gharama za uendeshaji kwani kuwa na serikali tatu kutasababisha
fedha nyingi kutumika kwa ajili ya gharama za uendeshaji kwa serikali hizo na
hivyo Taifa kuwa katika lindi la umasikini
Miongoni mwa wananchi wamependekeza serikali iangalie
uwezekano wa kubalisha katiba kwaupande wa dini kuhusiana na uhuru wa kuabudu
kutokana na madhehebu kurumbana juu ya nani ana haki ya kuchinja nasuala hilo
kuleta mkanganyiko hivyo wameitaka serikali moja kwa moja kuhusika na mabucha
Aidha wameitaka kipengele kiongezwe kuhusiana na usalama wa
waandishi wa habari na mali zao kulindwa ili kuhakikisha wanapewa ulinzi na
serikali wanapo tekeleza majukumu yao ya kikazi kutokana na waandishi kufanya
kazi katika mazingira hatarishi..
|
No comments:
Post a Comment