Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, September 4, 2013

Hatimaye mgogoro baina ya wanakijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI wilaya ya CHUNYA Mkoani MBEYA na jamii ya WAFUGAJI umemalizika baada ya serikali wilayani humo kuzikutanisha pande hizo na kuondoa tofauti zao.

 Baada ya mwenzao kuuwawa na maiti kuibwa hospitali wafugaji wakiandamana kuelekea eneo la tukio kujua kulikoni
Kazi kweli kweli
Mweyekiti wa kijiji  cha IGUNDU EMMANUEL MBUGHI akijaribu kuwatuliza wafugaji hao kuwa watulie na wakae chini na kujadili huo mgogoro wao
Hakika wafugaji wakatulia na kusubiri viongozi ili waanza kujadili swala lao
Afisa Tawala Wilaya ya CHUNYA AMIMU MWANDELILE ambaye alilaani vikali kitendo kilichofanywa na vijana hao kwani kitendo hicho hakikubaliki na jamii kwani kinaondoa utu wa Mtanzania.

Mwenyekiti wa Wafugaji SAMWEL LAURENT  akielezea jinsi mgogoro huo ulivyoanza
Baada ya majadiliano ya muda mrefu Mweyekiti wa kijiji  cha IGUNDU EMMANUEL MBUGHI alipatanishwa na Mwenyekiti wa Wafugaji SAMWEL LAURENT ambao walipatanishwa na Afisa Tawala Wa Wilaya ambapo pande hizo ziliahidi kukomesha vitendo hivyo na kwamba wananchi wa IGUNDU waondoe hofu wao kama wafugaji hawatalipiza kisasi na waendelee na shughuli za uzalishaji mali
Hakika hali ya amani imerejea tena sasa nifuraha tu



Hatimaye mgogoro baina ya wanakijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI wilaya ya CHUNYA  Mkoani MBEYA na jamii ya WAFUGAJI umemalizika baada ya serikali wilayani humo kuzikutanisha pande hizo na kuondoa tofauti zao.

Mgogoro huo uliodumu kwa wiki moja kufuatia baadhi ya vijana wa kijiji hicho kumuua mfugaji aliyefahamika kwa jina la SAID PETRO kwa kipigo kutokana na vijana hao kumtaka awape pesa naye kushindwa kutekeleza takwa lao ndipo walianza kumpiga.

Kabla ya kupatanishwa wafugaji hao walikutana faragha kutoa msimamo wao juu ya vitendo vilivyokithiri kutoka kwa wanakijiji cha IGUNDU wakidai hilo ni tukio la tano kutokea na serikali ya kijiji haijachukua hatua yoyote kukomesha vitendo hivyo.

Baada ya mjadala mrefu wafugaji walikubali kusogea meza ya mazungumzo yaliyoongozwa na Afisa Tawala Wilaya ya CHUNYA AMIMU MWANDELILE ambaye alilaani vikali kitendo kilichofanya na vijana hao kwani kitendo hicho hakikubaliki na jamii kwani kinaondoa utu wa Mtanzania.

AMIMU amesema vitendo vya uhalifu kijijini hapo vinachangiwa na unywaji wa pombe kupita kiasi na utumiaji wa madawa ya kulevya ambapo vijana wanatafuta njia ya mkato kutafuta pesa  ikiwemo kucheza kamali badala ya kufanya kazi.

Aidha amesema kuwa serikali haitafumbia macho vitendo hivyo atahakikisha wale wote waliohusika na vitendo hivyo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwani hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria hivyo anayevunja sheria hatavumiliwa kabisa.

Kwa upande wake AMIMU alichukua fursa hiyo kuwapongeza wafugaji hao kwa moyo wa uvumilivu kwa kutolipa kisasi pamoja na vitendo vya kikatili walivyofanyiwa wafugaji hao zaidi ya mara tano hata kupelekea wengine kujeruhiwa na wengine kuuawa.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu Mweyekiti wa kijiji  cha IGUNDU EMMANUEL MBUGHI alipatanishwa na Mwenyekiti wa Wafugaji SAMWEL LAURENT ambao walipatanishwa na Afisa Tawala Wa Wilaya ambapo pande hizo ziliahidi kukomesha vitendo hivyo na kwamba wananchi wa IGUNDU waondoe hofu wao kama wafugaji hawatalipiza kisasi na waendelee na shughuli za uzalishaji mali,

Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu

No comments: