Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, September 4, 2013

Wananchi waHALMASHAURI YA BUSOKELO Wilaya ya RUNGWE Mkoani MBEYA wajadili rasimu ya Katiba katika mchakato unaoendelea nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyokuwa ya kiraia inayojumuisha waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya inayojulikana kama ELIMISHA, kushoto  FESTO SIKAGONAMO amesema lengo ya asasi hiyo ni kuwapa fursa wananchi wa vijijini kuweza kutoa maoni yao katika mchakato wa Katiba


Wananchi waHALMASHAURI YA BUSOKELO Wilaya ya RUNGWE Mkoani MBEYA  wajadili rasimu ya Katiba katika mchakato unaoendelea nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyokuwa ya kiraia inayojumuisha waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya inayojulikana kama ELIMISHA, FESTO SIKAGONAMO amesema lengo ya asasi hiyo ni kuwapa fursa wananchi wa vijijini kuweza kutoa maoni yao katika mchakato wa Katiba

Baadhi ya wananchi wamependekeza serikali moja ya Muungano ili kupunguza gharama za uendeshaji kwani kuwa na serikali tatu kutasababisha fedha nyingi kutumika kwa ajili ya gharama za uendeshaji kwa serikali hizo na hivyo Taifa kuwa katika lindi la umasikini

Miongoni mwa wananchi wamependekeza serikali iangalie uwezekano wa kubalisha katiba kwaupande wa dini kuhusiana na uhuru wa kuabudu kutokana na madhehebu kurumbana juu ya nani ana haki ya kuchinja nasuala hilo kuleta mkanganyiko hivyo wameitaka serikali moja kwa moja kuhusika na mabucha

Aidha wameitaka kipengele kiongezwe kuhusiana na usalama wa waandishi wa habari na mali zao kulindwa ili kuhakikisha wanapewa ulinzi na serikali wanapo tekeleza majukumu yao ya kikazi kutokana na waandishi kufanya kazi katika mazingira hatarishi..


No comments: