Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, July 25, 2013

TBL YATOA SHIL. MILIONI 24 KUSAIDIA UJENZI WA KISIMA CHA MAJI KITUO CHA AFYA TUNDUMA MBEYA

Meneja kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala kulia akimkabidhi mfano wa Hundi ya shilingi milion 24 mkandarasi wakisima hicho Bwana Laurendt Ndelwa
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa mji mdogo Tunduma Rita Kamenye akiwashukuru kampuni ya TBL kwa msaada wa ujenzi wa kisima hicho kikikamilika kitasaidia sana katika kituo hicho cha afya kwani kina uhaba mkubwa sana wa maji
Mganga mfawidhi kituo cha afya Tunduma Dr Musa Mwakalyelye akisoma taarifa fupi ya kituo hicho
Baadhi ya ya wageni toka TBL na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya wakishuhudia tukio la kupewa mfano wa hudi kwa mkandarasi atakaejenga kisima hicho
Meneja kiwanda cha kampuni ya TBL Bia Mbeya Nicolaus  Kanyamala akitia saini kwenye hundi
Meneja uhusiano Dorris Malulu akitia saini  hundi 
 Meneja uhusiano toka TBL Dorris Malulu amesema kuwa TBL imekuwa na sera ya kusaidia maeneo mbali mbali hapa nchini kupitia faida kidogo inayopata kwa kuamua kurudisha sehemu ya faida hiyo kwa wananchi baada ya kubaini uhitaji wa msaada eneo husika, ambapo pamoja na mambo mengine meneja huyo alitoa rai kwa jamii kuona umuhimu wa kuisaidia serikali hapa nchini.


Meneja kiwanda cha kampuni TBL  Bia Mbeya Nicolaus  Kanyamala akiongea na baadhi ya maafisa wa mji mdogo Tunduma
Mara baada ya makabidhiano ya hundi wafanyakazi wa TBL walitembezwa katika kituo hicho cha afya kujionea wenyewe adha ya maji kituoni hapo
Hapa ni mahala pa kunawia kwenye chumba cha kujifungulia watoto

Picha na Mbeya yetu

No comments: