Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, July 24, 2013

MFUMO MPYA WA USAJILI WA VIZAZI KUPITIA MKAKATI WA USAJILI WA WATOTO WALIO NA UMRI CHINI YA MIAKA MITANO WAZINDULIWA MBEYA


 Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki akizindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,

Mgeni Rasmi,  Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki akimkabidhi mmoja wa akina mama Fides Samson akikabidhiwa cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake mwenye umri chini ya miaka 5,mara baada ya kuzindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,uzinduzi huo umefanyika kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,jijini Mbeya. Mpango huo umefadhiriwa na mashirika mbalimbali likwemo shirika la UNICEF,DFTDA (iliyokuwa CIDA Canada zamani) pamoja na Shirika la Wafanyakazi la kujitolea (VSO).
Baby TOT wakitumbuiza katika uzinduzi huo
Wakuu wa wilaya wa mkoa wa Mbeya
Makatibu tawala wa wilaya za Mbeya
Wakina mama na watoto walishiriki katika uzinduzi huo
Makirikiri ya Mbeya
Watoto wakifurahia na kucheza nyimbo zilizokuwa zinaimbwa navikundi mbalimbali vya sanaa
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wananchi wa mkoa wa Mbeya katika uzinduzi huo 
.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri RITA, Vicent Mrisho amesema kuwa, kutokana na kuwepo kwa takwimu zisizoridhisha za kumbukumbu za vizazi mwaka 2011, RITA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ilibuni mkakati wa usajili wa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano wenye lengo la kuboresha hali ya usajili nchini na kuweka kipaumbele kwa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano bure.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini,Dkt.Norman Sigalla akimkaribisha mgeni rasmi aongee na wananchi wa mkoa wa Mbeya
Afisa Mtendaji mkuu Rita Philip Saliboko risala Mbele ya mgeni rasmi
Mweshimiwa mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akisalimia wananchi katika uzinduzi huo
Mbunge wa Mbeya vijijini Mchungaji Lakson mwanjali akisalimia wananchi
Mwakilish toka Canada
Mwakilishi toka VSO
Mwakilishi toka TigoWoinde Shisael
Baadhi ya akina mama na watoto wao wakiwa pamoja na mgeni rasmi
Picha ya pamoja na maafisa wa RITA

Picha na Mbeya yetu

2 comments:

Gwanka said...

Picha ni nzuri na ni za kiwango kweli kweli. Hata hivyo nafikiri wasomaji hatujapewa vizuri habari yenyewe..Yaani huo 'mfumo mpya' au walau huo 'mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5'. Mkakati wenyewe ukoje?

Vinginevyo pongezi kwa jitihada za kuhabarisha.
Gwankaja.

Anonymous said...

I hope hizo pesa zitatumika ipasavyo kuboresha chumba cha kujifungulia watoto, inasikitisha.