Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, April 26, 2013

Wafanyabiashara wa soko la Ilomba jijini Mbeya wameandamana hadi kituo cha Polisi Ilomba Mbeya kwa madai ya kutaka mwenzao aliyekamatwa na kufikishwa kituoni hapo achiwe huru .

Wafanyabiashara wa soko la Ilomba Mbeya wakiwa nnje ya kituo cha polisi ilomba wakisubiri mwenzao aachiwe huru kwani hana makosa

Moja ya wafanyabiashara wa soko la Ilomba akiongea na mwandishi wa Mbeya yetu


Bado hali haieleweki kama mwenzao ataachiwa bado wapo kwenye mjadala na viongozi wao wa soko

Hatimae kiongozi wa pilisi wilaya kufika wafanyabiashara hao wanasubiri jibu toka kwa kiongozi huyo wa polisi


Hatimae mwenzao aachiwa huru ni vifijo na vigeregere kituoni hapo


Haoo wanaondoka kurudi kwenye soko lao huku wakiwa wanashangilia kuwa kamanda wao ameachiwa


wakivuka barabara kuu ya kuelekea tunduma


Kituo cha polisi ilomba sasa shwali baada ya kuondoka umati wa wafanyabiashara wa soko la ilomba

sokoni ilomba sasa hali imeanza kurejea kama kawaida baada ya soko hilo kufungwa kwa muda

Shangwe zinaendelea sokoni hapo baada ya kuachiwa kwa mwenzao

Kiduku mtindo mmoja sokoni hapo




Ndugu Tulizo Mbilinyi mwenye fulana nyeusi ndie alietuhumiwa kuiba mchele sokoni hapo 


 Mwenyekiti wa soko Ilomba Ndugu Athumani Kalonga amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni mmoja wa mfanyabiashara mwenzao ambaye ni kiongozi wa ulinzi sokoni hapo Ndugu Tulizo Mbilinyi kukamatwa na kufikishwa kituo hicho cha Polisi kwa madai kuwa ameiba mchele sokoni hapo.





Wafanyabiashara wa soko la Ilomba jijini Mbeya  wameandamana hadi kituo cha  Polisi Ilomba kwa madai ya kutaka mwenzao aliyekamatwa na kufikishwa kituoni hapo achiwe huru .
  
Kwa muda wa takribani masaa 3 kundi la wafanyabiashara wa soko hilo walifika kituoni hapo ambao wengi wao wakiwa ni akina mama wakidai kuwa mwenzao aliyekamatwa kwa tuhuma za  kuiba mchele wa mfanyabiashara mwenzake sokoni hapo   achiwe huru kwa madai kuwa mtu huyo si mhusika na tukio hilo la wizi.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa kituo cha Polisi Ilomba ambaye jina lake halikufahamika mara moja aliamua kuchukua maelezo ya pande zote mbili kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa ambapo baadae mtuhumiwa huyo aliachiwa huru na kuondoka kituoni hapo huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wafanyabiashara hao.

Akizungumzia kuibuka kwa mgogoro huo Mwenyekiti wa soko hilo Ndugu Athumani Kalonga amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni mmoja wa mfanyabiashara mwenzao ambaye ni kiongozi wa ulinzi sokoni hapo Ndugu Tulizo Mbilinyi kukamatwa na kufikishwa kituo hicho cha Polisi kwa madai kuwa ameiba mchele sokoni hapo.

Amesema suala hilo limeibua mkanganyiko mkubwa kwani mtu aliye husika  na kukamatwa kwa  kiongozi huyo ni mfanyabiashara mwenzao ambaye hakufuata taratibu zilizopo sokoni hapo hadi kufikia kumkamata mtu huyo.

Amesema taarifa za kuibiwa kwa mchele huo sokoni ziliwahi kutokea sokoni hapo lakini hazikuwahi kufikishwa ofisini hapo hivyo anashangazwa na hatua iliyochukuliwa na mwenzao kumchukua mtu huyo na kumfikisha kituoni.

Hata hivyo Kiongozi huyo wa soko analishukuru jeshi hilo la Polisi kuamua kmuachia mtu huyo kwani kungeweza kutokea mtafaruku mkubwa katika eneo hilo.

Pamoja na mfanyabisahra mwenzao kuachiwa wameamua kukakaa kikao cha pamoja na viongozi wote wa soko kwa lengo la kumaliza kabisa uhasama uliopo katika mlalamikaji ambaye jina lake halikufahamika (Mwanamke) pamoja na mtuhumiwa ili kuendela kuleta amani sokoni hapo.

1 comment:

Anonymous said...

Haki haiombwi Bali Inapiganiwa na Uoga ni Dhambi kubwa sana. Amani ya nchi inapatikana kwa Kupiganiwa.