Mwenyekiti wa soko Ilomba Ndugu Athumani Kalonga amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni mmoja wa mfanyabiashara mwenzao ambaye ni kiongozi wa ulinzi sokoni hapo Ndugu Tulizo Mbilinyi kukamatwa na kufikishwa kituo hicho cha Polisi kwa madai kuwa ameiba mchele sokoni hapo.
Wafanyabiashara wa soko la Ilomba jijini
Mbeya wameandamana hadi kituo cha Polisi Ilomba kwa madai ya kutaka
mwenzao aliyekamatwa na kufikishwa kituoni hapo achiwe huru .
Kwa muda wa takribani masaa 3 kundi la
wafanyabiashara wa soko hilo walifika kituoni hapo ambao wengi wao wakiwa ni
akina mama wakidai kuwa mwenzao aliyekamatwa kwa tuhuma za kuiba mchele
wa mfanyabiashara mwenzake sokoni hapo achiwe huru kwa madai kuwa
mtu huyo si mhusika na tukio hilo la wizi.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa kituo cha Polisi
Ilomba ambaye jina lake halikufahamika mara moja aliamua kuchukua maelezo ya
pande zote mbili kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa ambapo baadae mtuhumiwa
huyo aliachiwa huru na kuondoka kituoni hapo huku akishangiliwa na umati mkubwa
wa wafanyabiashara hao.
Akizungumzia kuibuka kwa mgogoro huo Mwenyekiti
wa soko hilo Ndugu Athumani Kalonga amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni mmoja
wa mfanyabiashara mwenzao ambaye ni kiongozi wa ulinzi sokoni hapo Ndugu Tulizo
Mbilinyi kukamatwa na kufikishwa kituo hicho cha Polisi kwa madai kuwa ameiba
mchele sokoni hapo.
Amesema suala hilo limeibua mkanganyiko mkubwa
kwani mtu aliye husika na kukamatwa kwa kiongozi huyo ni
mfanyabiashara mwenzao ambaye hakufuata taratibu zilizopo sokoni hapo hadi
kufikia kumkamata mtu huyo.
Amesema taarifa za kuibiwa kwa mchele huo sokoni
ziliwahi kutokea sokoni hapo lakini hazikuwahi kufikishwa ofisini hapo hivyo
anashangazwa na hatua iliyochukuliwa na mwenzao kumchukua mtu huyo na
kumfikisha kituoni.
Hata hivyo Kiongozi huyo wa soko analishukuru
jeshi hilo la Polisi kuamua kmuachia mtu huyo kwani kungeweza kutokea mtafaruku
mkubwa katika eneo hilo.
Pamoja na mfanyabisahra mwenzao kuachiwa
wameamua kukakaa kikao cha pamoja na viongozi wote wa soko kwa lengo la
kumaliza kabisa uhasama uliopo katika mlalamikaji ambaye jina lake
halikufahamika (Mwanamke) pamoja na mtuhumiwa ili kuendela kuleta amani sokoni
hapo.
|
1 comment:
Haki haiombwi Bali Inapiganiwa na Uoga ni Dhambi kubwa sana. Amani ya nchi inapatikana kwa Kupiganiwa.
Post a Comment